BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS JAKAYA KIKWETE APONGEZWA KWA KUANDIKIWA WARAKA NA MWENYEKITI WA UNGO MOROGORO.



WARAKA WA MARUPU KWA  MH.RAIS JAKAYA KIKWETE NA WATANZANIA.
Mwenyekiti wa Ungo Maliki Malupu.


Natumia fursa hii kuwasilisha waraka wangu kwa Mh Rais wa Jamhuri Ya Muungano Mh Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na mchakato mzima wa kuwapata wawakilishi wa Bunge la Katiba.

Natumia fursa hii kuwapongeza wajumbe wote walioteuliwa na Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXEDOxyair-bkUq_EmX0w_MV8C-XXJf4RNI6OAmsgNdKGB0p0y1XA8NGC7ZgiErSXv2rkaLUvUcqYR8zGWifXVwQt_kkUZ_9lrzV_KR5YZElOAebWozkfidY_wUC8PdFKYkCfg__ChOc4/s1600/1381392_667910669893509_1506018036_n.jpg 
RAIS KIKWETE.
 
Lakini nitoe pongezi zangu za dhati kwa Jukwaa la Katiba kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuwaunganisha pamoja wana AZAKI kwa ajili ya kufanya mchakato wa kuwapata wawakilishi wa AZAKI nchi nzima katika uchaguzi uliofanywa siku ya tarehe 30/12/2013  Dodoma.Lakini pia tunawashukuru The Foundation  For Civil Society kwa kazi kubwa kufadhili mkutano wa kupata wawakilishi katika Bunge la katiba pitia AZAKI

Natumia fursa hii kuwataka Watanzania kuwa na imani kubwa na wajumbe wote walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na tuwape ushirikiano wa hali na mali ili kuijenga nchi yetu ya Tanzania. Tunatoa wito kwa wajumbe wote wanaowakilisha Asasi za Kiraia kujua mambo ya msingi yafuatayo:-
(a)          Utaifa haujengwi na idadi ya serikali ila unajengwa kwa uimara wa serikali. Hivyo ni jambo la muhimu sana na kutafakari kwa kina ni muundo upi ni sahihi kwa ustawi wa Tanzania ya kesho.
(b)          
 Matatizo na kero zote za muundo wa serikali wabunge wajadili kwa maslahi ya kesho. Tunaweza pata katiba mpya leo baada ya muda wananchi wakadai katiba nyingine tena.

Na nakuunga mkono sana Mheshimiwa Rais kwa kulisisitiza suala la mjadala wa rasimu kuwa wa  hoja. Changes are not development but development are changes(Wilson chuchill).Katiba mpya si muungano tu tunamambo mengi sana ya msingi ya kujadili sio muungano tu.


(c)          Natumia fursa hii kuliweka wazi suala linaloibuliwa na baadhi ya Watanzania wenzetu wasioutakia wema undugu wetu wa kitaifa kuhusu kudai 14km kutoka usawa wa bahari kuelekea nchi kavu kuwa ni eneo la Zanzibar kwa mujibu wa mkataba wa Sultan Seid Said na serikali ya Muingereza mwaka 1849.

 Mkataba ule  ni aibu kuutamka kwa maana ulikuwa na vifungu 14 kifungu namba 4 cha mkataba huo kinasema “Zanzibar will be Slave Centre for life” kwa mujibu wa kifungu hiki sina cha kuongeza hata kidogo juu ya suala hilo. Lakini pia mkataba wa Sultan na Uingereza hauwahusu watanzania hata kidogo kwa maana mkataba ule ulifanyika Oman. Kitu kingine wakati mkataba unasainiwa Tanganyika haikuwa koloni la waingereza.Sisi ni wamoja na ndugu wa kweli tusitenganishwe na utashi.


Lakini nataka nitoe wito kwa Wabunge vijana uliowateuwa  katika Bunge la Katiba watambue kuwa wana dhamana kubwa kuliko thamani na heshma walionayo kwa sasa. Vijana wanaohitimu ngazi ya cheti hadi uzamivu ni milioni moja na lakini mbili 1,200,000 kwa mwaka kwa mwaka wa masomo 2012-2013.Wakati mwaka 1961 wahitimu walikuwa 14 tu.Lakini wanaopata ajira rasmi ni vijana laki mbili tu 200,000 tu

 Ni mafanikio makubwa sana yaliyopatikana Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kazi  yake imeishia hapo nyinyi kama vijana mliomo katika Bunge la katiba mnatambua nyie ndio mtakaounda katiba itakayopelekea mabadiliko ya sheria na sera za ajira.


Tunatoa wito kwa vijana wote kuthamini maisha ya vijana wenzenu mliowaacha na elimu zao za cheti na shahada hawajui wataanzia wapi huku wakisubiri wapate uzoefu wa miaka mitano (5) ili waajiriwe. 


Lakini pia muundo wa kijiografia Mh Rais ni muhimu Bunge liutazame kwa mapana sana mfanano visiwa tulivyonavyo Tanzania havitendewi haki hata kidogo Mfano mzuri ni kisiwa cha ukerewe chenye ukubwa wa wastani wa 6640 kirometa za mraba kina visiwa 14 vinavyokaliwa na watu wasiopungua elfu ishirini kila kisisiwa.


Kisiwa kama hiki kubaki kuwa wilaya hatuwatendei haki hata kidogo sambamba na kisiwa cha Mafya ambao huduma za kimkoa zinapatikana kabaha Pwani ni mateso makali wanayoyapata Watanzania hawa.


Mh Rais katika mabadiliko ya katiba lazima yazingatie uiano wa kijiografia  sambamba na mahitaji ya kweli ya Watanzania.Pia sera ya Wazee waliostaafu kuangalia maslahi yao ikiwa ni pamoja na kulipwa stahiki zao zinazokidhi mahitaji yao ya msingi kwa kila mwezi badala ya  kulipwa kila baada ya miezi mitatu.


Mabadiliko ya katiba lazima yasadifu stahili hizi za watumishi waadilifu wastaafu

Natoa wito kwa wajumbe ambao hawakupata bahati ya kuchaguliwa wasikate tamaa safari ya mafanikio haianzi kwa mafanikio.Mjitahidi kuwajibika ipasavyo katika majukumu yetu na mafanikio yatapatikana. 


Pia vijana mnapaswa kuhakikisha mnajitokeza kujiandikisha katika daftari la kujiandikisha kupiga kura na mnagombea nafasi mbalimbali kuanzia vitongoji na mitaa/kijiji wakati utakapo wadia kwa mujibu wa maelekezo yatakavyotolewa na tume huru ya uchaguzi. 


Zindukeni mbadili maisha yenu sasa. Huu ndio wakati wenu vijana kutoa maisha yenu kwa ajili ya taifa letu nguvu kazi yenu ndio msingi wa Tanzania mpya maisha yetu hayawezi kubadilishwa bila kuzinduka, kujitoa na kuwajibika kwa ajili ya nchi yetu amka kijana zinduka pambana tuushinde umasikini na ujinga.


Tusijisifu kwa   familia zetu kuwa maskini tuupige vita umaskini.Na tusiendelee kuwategemea wastaafu (retired officers) kuendelea kutuongoza sisi kama vijana tuamke sasa tuseme.


 Mwisho mh.Rais nakutakia afya njema katika ujenzi wa taifa letu huru Tanzania karibu  sana UNGO Morogoro.

Nawashukuru wana morogoro kwa ushirikiano wenu mlioutoa wakati wote katika mchakato wa kupata wawakilishi katika bunge la katiba asanteni sana nawashukuruni sana.Naomba kuwasilisha waraka


WARAKA HUU UMETOLEWA NA
Maliki s. Marupu
Mwenyekiti wa  Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Morogoro (UNGO).


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: