BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC YAIHESHESHA OLJORO JKT UWANJA WA TAIFA NA KUITANDIKA BAO 4-0, AMIS TAMBWE AMTUNGUA KIPA MARA 3.

Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe (katikati) akiwatoka mabeki wa Oljoro JKT, Aziz Yusuf (chini), Nurdin Mohamed (kulia) na Sabri Makame wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara, kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Simba ilishinda 4-0. Picha na Michael Matemanga.


Mshambuliaji Amis si Tambwe amefunga mabao matatu peke yake na kuisaidia Simba kuisambaratisha Oljoro JKT 4-0 jana katika mechi ya Ligi Kuu bara iliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mrundi huyo anayeongoza kwa ufungaji mabao kwa sasa alifunga mabao yake katika dakika ya 20, 27 na 50 baada ya kiungo Jonas Mkude kupachika bao la kuongoza dakika ya 12.
Kwa mabao hayo, Tambwe amefikisha mabao 13 na kuweka rekodi ya kufunga mabao matatu katika mechi moja kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo kwenye mzunguko wa kwanza katika mchezo dhidi ya Mgambo JKT wakati Mrundi huyo alipofunga mabao manne huku Simba ikishinda 6-0.
Rekodi ya juu ya kufunga mabao mengi katika mechi moja ya Ligi Kuu bara bado inashikiliwa na mchezaji wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila aliyefunga mabao sita peke yake wakati Yanga ilipoisambaratisha RTC Kagera 8-0 mwaka 1998.
Simba sasa imefikisha pointi 30, ambapo leo itaomba wapinzani wake Yanga (32) na Mbeya City (31) watoke sare pia wakiomba Azam yenye pointi 33 wapoteze mechi yao dhidi ya Kagera Sugar ili kufanya tofauti ya pointi baina yao kuwa ndogo.
Simba waliuanza mchezo wa jana kwa kasi na dakika ya 12, kiungo Mkude alifunga bao la kuongoza kwa kuunganisha vizuri krosi ya Ramadhani Singano.
Kama hiyo haitoshi, Singano aliwatoka mabeki wa Oljoro na kupitisha krosi safi kwa Tambwe ambaye hakufanya makosa kwani alipiga shuti na kufunga bao la pili katika dakika ya 20.
Baada ya kufungwa mabao hayo, viungo, mabeki pamoja na kipa wa Oljoro Mohamed Ally walionekana kukosa mwelekeo, ambapo uzembe wa viungo wa Oljoro ulitoa mwanya kwa Haruna Chanongo kuchomoka na mpira katikati ya uwanja na kupiga pasi ndefu kwa Tambwe aliyempiga chenga beki na kupiga shuti kuandika bao la tatu dakika ya 27.
Mrundi huyo aliendelea kuwa mwiba kwa kwa ngome ya Oljoro kwa kupachika bao la nne akimalizia pasi ya Mkude katika dakika ya 50.
Akizungumza baada ya mechi hiyo kumalizika, Kocha wa Oljoro, Hemed Morocco alisema,”Simba walistahili kushinda kwa sababu wachezaji wangu walipoteza umakini uwanjani.”
Katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, jahazi la Ashanti United limezidi kuzama baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mgambo Shooting.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: