BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM YASITISHA KAMPENI ZA UBUNGE MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA ILI KUSHIRIKI MAZISHI YA WATU WATATU WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI IRINGA.


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa kikifanya kampeni katika kijiji cha Kidamale Jimbo la Kalenga, kimelazimika kusitisha kampeni zake kwa muda ili kushiriki maziko ya watu watatu waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika jimbo hilo.

Ajali hiyo ilitokea juzi kwa kuhusisha gari la kiwanda cha kusambaza maji ya Afrika cha mkoani humu aina ya Isuzu Foward lenye namba za usajili T 750 AFJ. Aidha, ajali hiyo pia ilisababisha watu wanne kujeruhiwa. Waliokufa katika ajali hiyo ni Nyagile Luvanda (38), Sabasaba Kunzugala (35) na Anskali Chengula (20), wote wakazi wa kijiji cha Kidamali. 


Majeruhi ni Shukuru Msigwa (20), Riziki Kyando (30), Jimmy Luvanda (21) na Spedito Mgongolwa (28), wote wakazi wa kiojiji cha Kidamali. Majeruhi hao walipelekwa katika hospitali ya Tosamaganga kwa matibabu. 



Akiongoza maziko hayo juzi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, alisema CCM imepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na ndiyo maana wamelazimika kusitisha kampeni hizo na kushiriki kwenye maziko.


Nchemba kwa niaba ya CCM alitoa Shilingi milioni moja kwa familia za marehemu hao huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tawi la Kidamali, waklitoa Sh. 50,000. Miili ya marehemu hao ilizikwa katika makaburi ya kijiji cha Kidamali.
Aidha, Nchemba alisema kuwa endapo CCM itapewa ridhaa ya kuongoza katika jimbo hilo, mgombea wao Godfrey Mgimwa, atasaidia watoto walioachwa na marehemu William Mgimwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: