BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHADEMA IJIPANGE UPYA KATIKA KINYANG'ANYIRO ZA UCHAGUZI, YAAMBULIA KUSHINDA KITUO KIMOJA UCHAGUZI WA KALENGA IRINGA, CCM YAENDELEZA UBABE KWA CHADEMA KALENGA TENA.

Polisi akilinda Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Chekechea ya Mchwivila katika Jimbo la Kalenga, Iringa jana . Picha na Edwin Mjwahuzi.

KALENGA.

MGOMBEA wa CCM, Godfrey Mgimwa anaonekana kufanya vizuri katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika jana katika Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.
Mgimwa aliwaacha mbali mshindani wake wa karibu, Grace Tendega wa Chadema na Richard Minja wa Chausta.


Kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM katika sehemu mbalimbali za jimbo hilo na Mjini Iringa walikuwa wakishangilia kile walichokiita ushindi wa kishindo.


Watu 71, 765 walitarajiwa kupiga kura katika vituo 216, lakini waandishi wa Mwananchi walisema kulikuwa na idadi ndogo ya watu waliojitokeza katika baadhi ya vituo, huku wengi wakilalamika kushindwa kupiga kura kutokana na kupoteza vitambulisho.


Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa 10:00 na kazi ya kuhesabu kura ilianza mara moja na matokeo yalianza kubandikwa kwenye vituo husika kuanzia saa 11:00 jioni huku CCM kikionekana kufanya vizuri kuliko vyama vingine.


Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Kalenga, Purdenciana Kisaka alisema uchaguzi ulifanyika kwa ufanisi... “Mimi na timu yangu hivi sasa tunajiandaa kupokea masanduku ya kura, ili tujumlishe na kuona kile kilichomo. Tutatangaza matokeo mapema kadiri inavyowezekana,” alisema Kisaka.


Matokeo ambayo yalikuwa yamebandikwa vituoni na kunukuliwa na waandishi wetu ni kama ifuatavyo:


Kata ya Ifunda:
Kituo cha Zahanati ya Kibena na. 1; CCM 93, Chadema 36, Chausta 2, Zahanati na.2: CCM 91, Chadema 28, Chausta 0, Shule ya Msingi Kibena CCM 91, Chadema 23, Chausta 0, Ofisi ya Kijiji Ifunda A; CCM 84, Chadema 73, Chausta 1, Kituo B; CCM 75, Chadema 76, Chausta 0.


Kituo cha Kivalali Nyumba ya Mifugo na. 2; CCM 109, Chadema 14, Chausta 1, Kivalali na. 1: CCM 99, Chadema 19, Chausta 1, Kilimahewa B Ofisi ya Kitongoji; CCM 57, Chadema 32, Chausta 1.


Kata ya Maboga:
Kijiji cha Makongati Kituo cha Josho, CCM 120, Chadema 13, Chausta 1, Shule ya Msingi Makongati; CCM 160, Chadema 9, Chausta 2,Kijiji cha Kiponzelo, Kituo cha Msombe; CCM 98, Chadema 13, Chausta 0, Shule ya Msingi Kiponzelo; CCM 45, Chadema 5, Chausta 1.MWANANCHI

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: