TUKIO LA BASI LA YANGA KUPATA AJALI HIVI NDIVYO ILIKUWA HEKA HEKA ZAKE MIKESE.
Askari wa usalama barabara akisimamia zoezi la wachezaji kuchukua mabegi yao kuhakikisha usalama unakuwepo hasa kwa kusimamisha magari yaliyokuwa yakipita barabara hiyo.
Kocha mkuu wa Yanga Hans na msaidizi wake Boniface Mkwasa kulia na daktari wa timu hiyo wakiwa wameka wakati wakisubiri usafiri mungine wa kujerea jijini Dar es Salaam.
MLOLONGO wa matukio ya Yanga kwenye mechi za Morogoro tangu mwaka 2009 umeshtua uongozi pamoja na benchi la ufundi ambalo limesisitiza kwamba lazima kitu kifanyike.
Mbaya zaidi jana Jumapili asubuhi wakati wanarejea Dar es Salaam walipata ajali maeneo ya Mikese, Morogoro na kunusurika kuumia.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm licha ya kulalamikia hadharani uduni wa Uwanja wa Jamhuri, lakini baadaye alikaa na vijana wake kwa nyakati tofauti na kuwalaumu kwa kushindwa kulazimisha pointi tatu kwenye uwanja huo na kuiacha Azam ikipepea kileleni mwa msimamo.
Kwa mujibu wa rekodi za Ligi Kuu Bara tangu mwaka 2009, Yanga haijawahi kuifunga Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro huku kukiwa na matukio kadhaa ya utata timu hizo zinapokutana.
Yanga iliifunga Mtibwa uwanjani hapo mabao 2-1 mwaka 2009 na tangu hapo, Wanajangwani hawajawahi kupata ushindi mwingine wowote katika mechi ilizocheza Jamhuri licha ya sapoti kubwa ya mashabiki wa mji huo wenye watu zaidi ya milioni 2.2 kwa mujibu wa takwimu za mwaka juzi.
Katika michezo mitatu iliyozikutanisha timu hizo Morogoro tangu mwaka 2010, Yanga imeambulia kipigo kimoja na sare mbili pekee. Yanga ilitoka sare ya 1-1 Septemba 2010, pia ilitoka suluhu Septemba 2011 kabla ya kufungwa mabao 3-0 Septemba 2012.
Mtibwa iliifunga Yanga bao 1-0 Februari 2011 ikiwa ni ushindi pekee katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano.
Yanga katika kipindi cha miaka mitano imeshinda michezo minne dhidi ya Mtibwa Dar es Salam huku ikipata sare mbili katika michezo mingine Dar es Salaam. Ushindi mkubwa Yanga ilioupata nyumbani ni wa mabao 3-1 mara mbili tofauti Februari 2010 na 2012.
Kuhusu Yanga kutofanya vizuri dhidi ya Mtibwa tangu 2009 mjini Morogoro baadhi ya wadau wa soka wanasema ni hali ya kisaikolojia inayowakuta wachezaji wa Yanga kila wanapokaribia mechi hiyo.
Kocha Mtibwa
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, alisema; “ kuwa Yanga wanashindwa kufanya vizuri katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa sababu wanakuwa na papara.”
“Yanga ni timu nzuri ila wanapokuja Morogoro wanakuwa na papara ya kutaka kushinda, matokeo yake wanashindwa kufanya hivyo. Yanga watatufunga wakiwa Dar es Salaam, Jamhuri huwa inawasumbua ndiyo maana wanapata matokeo mabovu, wao wamezoea viwanja vya Dar es Salaam,” alisema Maxime. MWANASPOTI.
0 comments:
Post a Comment