Na Juma Mtanda, Morogoro.
KOCHA mkuu wa klabu ya Kimondo FC ya mkoa wa Mbeya, Marthin Maimbo amelazimika kuingia uwanjani wakati mchezo ukiendelea kutuliza jazba za wachezaji wake zilizozuka baada ya mlinda mlango wa klabu hiyo, Abraham Simasiku kupewa kadi nyekundi na kutolewa nje ya uwanja katika mchezo baina ya timu hiyo na wenyeji wao Burkina FC katika ligi daraja la kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.Tukio hilo lilitokea dakika ya 80 baada ya Mlinda mlango wa klabu hiyo, Abraham Simasiku kumchezea vibaya mshambuliaji wa Burkina FC, Mrisho Said eneo la hatari huku filimbi ya mwamuzi Allanus Luena kutoka Mwanza ikiwa tayari imepulizwa kuashiria kutendeka kwa madhambi katika lango lao.
Golikipa huyo namba moja alifanya madhambi hayo na mwamuzi wa mchezo huo kutoa adhabu ya kadi nyekundu na penalti hali iliyooenekana wachezaji wa Kimondo kukerwa na adhabu hizo na kuanza kumzonga mwamuzi na kumtaka kumpiga huku nahodha wao akituliza jazba za wachezaji hao bila mafanikio.
Hali hiyo ilimlazimisha kocha huyo kuingia uwanjani kutuliza jazba za wachezaji wake dakika ya 80 ili kunusuru kuepukana na adhabu kutoka ndani ya shirikisho la mpira Taznania (TFF) za kuanzisha vurugu mchezoni na kumwingiza mlinda mlango namba mbili kuziba pengo hilo.
Mshambuliaji wa Burkina FC, Mrisho Said alitumia vema adhabu hiyo na kuipatia timu yake bao pekee katika mchezo huo na kuifanya kufikisha pointi 14 huku ikiwaacha Kimondo FC ikiwa na pointi zake 10 wakati katika mchezo mungine wa ligi hiyo Mkamba Rangers ya Morogoro ililazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Mlale JKT mchezo uliofanyika uwanja wa CCM Mkamba Morogoro.
Vinara wa kundi hilo Polisi Moro SC wenye pointi 19 ilishuka dimbani jana uwanja wa jamhuri kuonyeshana kazi na Kurugenzi ya Mufindi yenye pointi 16 katika ligi hiyo huku JKT Mlale ikiwa na pointi 17, Kurugenzi Mufindi pointi 16, Burkina FC ikiwa na pointi 14, Lipuli ya Iringa yenye pointi 13 na Mkamba Rangers ikiburuza mkia kwa kuwa na pointi 10. CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment