BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC YAIBUKIA KWA RUVU SHOOTING, YAPATA USHINDI WA BAO 3-2 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.

Simba mpyaHatimaye baada ya vipigo vitatu na sare mbili klabu ya Simba leo imepata ushindi katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom.

Mchezo wa uliochezwa katika dimba la uwanja wa taifa baina ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting umeisha kwa matokeo ya 3-2.


Alikuwa yule yule bwana Amis Tambwe ambaye alianza kufungua kitabu cha mabao kwa upande wa Simba mwanzoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza la pili mwishoni mwa kipindi cha pili. Mpaka mpira unaenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao mawili kwa nunge.

Kipindi cha Ruvu Shooting walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika 70, dakika mbili baadae Haruna Chanongo akaongeza bao la 3 kwa Simba. Dakika ya 83 Ruvu wakafunga bao la pili kwa penati baada ya beki Joseph Owino kuunawa mpira kwenye boksi la penati. Ruvu waliendelea kulisakama lango la Simba lakini bahati haikuwa yao na mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalikuwa 3-2 – Simba wakitoka na ushindi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: