BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TUKIO LA KUSIKITISHWA !!! MWANAFUNZI NA MUOKOAJI WAFARIKI MAJI BAADA YA MTUMBWI WALIOKUWA WAKISAFIRIA KUPIGWA NA DHURUBA SINGIDA.

 
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Ipembe mjini hapa,Rashid Saidi (16) amefariki dunia baada ya mtumbwi aliokuwa umeupanda ziwani, yeye na baadhi ya wanafunzi wenzake kupigwa na upepo mkali na kusababisha mtumbwi kupinduka na wao kutumbukia kwenye maji. Kijana mmoja ambaye sio mwanafunzi na jina lake bado halijapatikana,alijitolea kumwokoa mwanafunzi huyo,lakini naye kwa bahati mbaya alifariki dunia baada ya kunywa maji mengi na kuzama ziwani.Tukio hilo la kusikitisha limetokea machi nane mwaka huu saa nane mchana.


Inadaiwa kuwa wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha’tuition’ shuleni kwao,kama kawaida yao walienda ‘pikiniki’ katika ziwa la Kindai na kuanza kuogelea pembeni mwa ziwa hilo.


Askari kutoka kikosi cha zima moto mjini hapa,Bahati Hemed,amesema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na mashuhuda wa tukio hilo,ni kwamba baada ya wanafunzi hao kumwagwa ndani ya maji,baadhi ya wanafunzi walifanikiwa kujiokoa na Rashid ambaye hana uzoefu wa kuogelea,alizama nada ya maji.


Amesema wanafunzi hao baada ya kutoka nje ya ziwa,walimwomba kijana mmoja ambaye alikuwa na umri mkubwa aingie ziwani ili akamwokoe mwanzao.

“Yule kijana aliyejitolea kumwokoa mwanafunzi, alipokaribia alikotumbukia mwanafunzi huyo, na yeye mambo yalimwendea vibaya na hivyo kutupikia ndani ya maji na kusababaisha na yeye apoteze maisha yake”alisema Bahati kwa masikitiko.

Alisema baada ya hapo waliweza kuita wavuvi ambao walifika na nyavu na kuwaza kutoa miili hiyo miwili kutoka ndani ya ziwa Kindai.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: