BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA !!! BADO KURA YA SIRI, WAZI BADO NI KAA LA MOTO KWAO.


Mjumbe wa Bunge maalumu la Katiba, Chritopher Ole Sendeka.

DODOMA. 
WAJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, juzi na jana wamekuwa katika mtihani mgumu wa kufikia uamuzi wa pamoja kuhusu utaratibu wa upigaji kura, kati ya kura ya wazi na kura ya siri.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilisema kutokana na mvutano huo, mjumbe mmoja, Chritopher Ole Sendeka, alijikuta akilia hadharani akitetea upigaji kura ya wazi.
Kikao hicho kilichofanyika juzi kati ya saa 2:00 na saa 5:30 usiku chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kilishuhudia mabishano makali kati ya wanaotaka kura ya siri dhidi ya wale wanaotaka kura ya wazi.
Habari hizo zilisema baada ya Pinda kufungua kikao hicho, alimkaribisha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Shamsi Vuai Nahodha, ili atoe mrejesho wa kikao cha mashauriano.
Inaelezwa kuwa katika kikao hicho, Nahodha aliwaambia wajumbe kuwa kutokana na mazingira yaliyopo ndani na nje ya Bunge kwa upande mmoja na wananchi kwa upande mwingine, kura ya siri haiepukiki.
“Kilio cha Ole Sendeka kwenye party cocas kikao cha chama (party cocus) juzi usiku kilitokana na kauli ya Nahodha kwamba kura ya siri haiepukiki,” alidokeza mbunge mmoja wa CCM aliyehudhuria kikao hicho cha faragha.
Mbunge huyo alilidokeza gazeti hili kuwa ndani ya kikao kulikuwa na mabishano makali baada ya kauli ya Nahodha, huku baadhi ya wabunge wakisema wananchi wamechoshwa na msimamo wa CCM.
Ni kutokana na mabishano hayo ndipo Ole Sendeka aliposimama akipinga mapendekezo yaliyotaka CCM kulegeza msimamo na kuridhia kura ya siri na wakati alipokuwa akizungumza alipobubujikwa na machozi.
Huku akilia katika kikao hicho, inadaiwa Ole Sendeka akisema kwamba kukubali kura ya siri ni kuitosa CCM na msimamo wake wa kutaka muundo wa Serikali mbili.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa Ole Sendeka alienda mbali zaidi na kusema endapo Pinda ataridhia kura hiyo ya siri, basi yeye (Pinda) na viongozi waandamizi wa CCM waliohudhuria watawajibishwa na CCM.
Kutokana na mtafaruku huo, kikao hicho kilishindwa kufikia mwafaka na kuahirishwa hadi jana saa 5:00 asubuhi ambapo hoja ya ama kura ya siri au ya wazi, iliendelea kuwagawa wabunge katika makundi mawili.
Wakati akifungua kikao cha jana, Pinda alisema kutokana na yaliyotokea katika kikao chao cha juzi usiku na baada ya kutafakari kwa mapana yake, chama kimeamua kibakie na msimamo wake wa kura ya wazi.MWANANCHI

 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: