Jerry Tegete (kushoto) akishangilia bao lake kwa staili ya kunong'oneza, huku akipongezwa na Simon Msuva (kulia) na Mrisho Ngasa. KLABU bingwa ya ligi kuu ya Vodacom Dar Young Africans leo imeendeleza ushindi katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom ambapo imefanikiwa kuifunga Rhino Rangers ya Tabora 3-0 kwenye game iliyochezwa Tabora. Mabao ya Yanga yalifungwa na Hussein Javu, Jerry Tegete na moja alijifunga mchezaji wa Rhino Labana.

0 comments:
Post a Comment