Mbali na watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi wa sasi hilo ambapo dereva wa alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na
kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ya kutokea kwa ajali hiyo basi hilo lilianza kuyumba na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara hiyo.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe alithibitisha kupokea majeruhi 60 pamoja na maiti 11.
Amesema kati ya majeruhi hao 25 hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo zinaendelea vizuri na tayari wengine wameanza kuruhusiwa.
Jeshi la polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment