BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDOA YA DIAMOND NA WEMA YAIVA, KUFUNGA PINGU ZA MAISHA AGOSTI 2014.

 
Wapendanao Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu katika pozi la kimahaba. 

MTABIRI mwenye jina kubwa kwa sasa Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Yahya Hussein ameibuka wiki hii na kuanika kwamba, Agosti mwaka huu Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu watafunga ndoa.
Akizungumza na Amani jijini Dar es Salaam juzikati, Hassan alisema amepiga mahesabu ya kinyota kwa wapenzi hao na kubaini kuwa, Agosti ndoa yao itafungwa mahali popote nchini Tanzania.

Akaongeza: “Kama wapo kwenye mipango au maandalizi wakazane, kwani mwezi Agosti ndiyo wenyewe kwa mujibu wa nyota za wote.
 

Wema.

“Lakini nawapa angalizo muhimu, wakae wakijua kwamba kama ndoa hiyo haitatimia Agosti kutokana na sababu zao wenyewe, haitafungwa tena hadi mwaka 2016, kwa sababu lazima ndoa yao iwe kwenye mwaka unaogawanyika.”
 

Diamond.

Maalim Hassan aliendelea kuweka wazi kwamba, vikwazo vyote ambavyo vilikuwa vikiwazunguka wawili hao, kwa mujibu wa nyota zao, vimetoweka, akimaanisha havipo tena.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: