BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MATUKIO YA MAKAMU WA RAIS, MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA KAMANDA KOVA MARA BAADA YA KUPATA AJALI HELIKOPTA HIVYO NDOVYO WALIVYOENDELEA NA KAZI ZAO JIJINI DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa maelekezo kwa katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Injinia Mussa Ibrahim Iombe wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, katikati ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadick.

Asubuhi April 13 2014 makamu wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Mecky Sadick na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dsm Suleiman Kova walipata ajali ya Helikopta iliyoanguka uwanja wa ndege Dar wakitaka kutembelea sehemu zilizo athirika na mafuriko.

Mwandishi mmoja aliekuepo kwenye ndege hiyo aliongea kwa ufupi na millardayo.com anasema wakati wanaanza kupaa, ni kama upepo mkali ulikua unaivuta Helikopta kurudi nyuma ikiwa imepaa urefu wa kama futi tano ambapo ilizidiwa nguvu na kugonga paa kisha ikaanguka.

Baada ya ajali walijitazama wakaona ni wazima isipokua michubuko midogomidogo kisha wakarudi kwenye magari yao na kuyatumia kuelekea moja kwa moja kwenye maeneo waliyokua wamepanga kwenda kwa Helikopta.

Makamu wa Rais akionyeshwa na katibu mkuu wa wizara ya ujenzi Injinia Mussa Iombe, sehemu ya daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam lililokatika kutokana na mvua kubwa.

Malori yakiendelea kumwaga vifusi vya mawe kwenye daraja hilo


Unataka kuwa karibu na kila tukio linaloifikia millardayo.com ? jiunge kwenye familia na niwe nakutumia zote kupitia twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo.

Nguzo za umeme baada ya kuzidiwa nguvu na maji yaliyobomoa daraja.



Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: