BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AFANDE SELE KUWASHA MOTO TAMASHA LA KUMBUKUMBU YA MANGWEA LA LOVE CONCERT UKUMBI WA NYUMBANI PARK MANISPAA YA MOROGORO.

 
Na Mtanda Blog, Morogoro.
Mkali wa rhymes Seleman Msindi a.k.a Afande Sele ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania katika muziki wa kizazi kipya wanaotarajia kutumbuiza katika tamasha maalum la Love Concert la kifo cha mwaka mmoja cha mwanamuziki marehemu Albert Mangwea  Ngwair  ambalo linafanyika ukumbi wa  Nyumbani Park Manispaa ya Morogoro mjini leo Juni 28 mwaka huu.


Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mjini hapa, Mratibu wa tamasha hilo, Kareeem Omary alisema kuwa Afande Sele ni miongoni mwa wanamuziki wa kizazi kipya watakao kutoa burudani katika tamasha hilo lililopewa jina la kumbukumbu ya kifo cha mangweir "Love Concert".

Kareem alisema kuwa licha ya Afande Sele kuthibitisha kutumbuiza katika tamasha hilo, wasanii wengine ni pamoja na P Funky Majani, , Belle 9, Mc Koba, Samir, JSqueezer, Mswaki, Team Racers, Chris wa Marya, Zombie, President  Mirrow,  Jordan wa Dejavu na wengine wengi.

“Tunataka kumuenzi Mangweir kwa kuwakusanya baadhi ya wasanii kutumbuiza katika tamasha la kumbukumbu ya kifo chake tangu kufariki dunia na sasa ni mwaka mmoja ambalo litakuwa linajulikana kama Love Concert na litafanyika kila mwaka.”alisema Kareem.

Kareem alisema kuwa anawaomba wadau wa muziki wa kizazi kipya na wengine kujitokeza kuonesha  upendo wao pamoja kama ilivyo utamaduni wa watanzania kukimbilia katika matukio ya namna hiyo.

Mama mzazi wa marehemu Mangwea atakuwepo kwenye tamasha hilo pamoja na kundi la Wanachemba ambalo pia aliwahi kufanya kazi na Mangweir ambapo tukio hilo linaenda sambasamba na siku ya Juni 28 ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu. Alisema Mratibu huyo.


Tamasha limeanza majira ya saa 10 alasili hadi saa 12 jioni ambapo watoto wameonyesha vipaji vyao vya muziki kwa kuimba huku saa 2 usiku ikitarajiwa wasanii kutumbuiza.

Mangweir aliwahi kuwika na vibao ikiwemo Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi na kushirikishwa na wasanii kama TID, Profesa Jay, Nuru, Chid Benz na wengine wengi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: