Klabu ya soka ya Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma imenusurika kupokea kichapo kutoka kwa African Sports FC ya Tanga huku Kiluvya FC ikiendeleza kugawa pointi katika ligi ya mabingwa wa mikoa inayoendelea kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 huku mshambuliaji, Hamis Wanyama akiinusuru klabu hiyo kupata kipigo hicho katika dakika ya 86 mkoani hapa.
African Sports ilipata bao lao la kuongoza dakika ya 36 kupitia kwa Ally Kagawa baada ya kuunganisha vema krosi ya Issa Yassin na kukwamisha mpira wavuni huku James Mendi akishindwa kuipatia klabu yake bao dakika ya 29 kufuatia mkwaju wake wa penalti kuota mbawa baada ya golikipa wa CDA kumfanyia madhabi Hassan Omari na mwamuzi wa mchezo huo, Athman Lazi kutoa adhabu hiyo.
Timu ya Kiluvya FC inayonolewa na kocha mkuu Yahaya Issa imeendeleza kugawa pointi katika ligi hiyo baada ya kukubali kutandikwa bao 3-1 kutoka kwa Mshikamano FC ya Dar es Salaam katika mchezo mkali uliochezwa majira ya saa 10 uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
MSHAMBULIAJI WA KILUVYA UTD, SAID MKINI AKIMTOKA JAMES SALU WA AFRICAN SPORTS KATIKA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA YA MIKOA KITUO CHA MORO.
Mshikamno FC ilianza kuhesabu kalamu ya mabao katika dakika ya saba baada ya Victor Hagaya kufunga bao la kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi ya Abas Mohamed huku Abas Mohamed akifumania nyavu kwa kufunga bao la pili kwa mpira wa adhabu ndogo uliotingisha nyavu kufuatia Bakari Bakari kufanyiwa madhambi katika dakika ya tisa.
Kiluvya FC walipata bao lao pekee katika dakika 68 lililokwamishwa wavuni na Omari Hussein kwa njia ya penalti baada ya mlinzi wa Mshakamono kufanya madhambi eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo, Marthin Saanya kutoa adhabu hiyo huku mshambuliaji Victor Hagaya akishindia msumari kwa kupachika bao la tatu na kufanya mchezo huo Kilivua kupoteza mchezo wa tatu mfululizo wa ligi hiyo iliyoanza mei 10 mwaka huu.
Katika michezo mingine Pachoto Stars FC ya Newala mkoani Mtwara ilipoteza kupoteza mchezo wake wa pili mbele ya Bulyanhulu FC kwa kufungwa bao 1-0.
Bao hilo la Bulyanhulu FC lilifungwa na mshambuliaji Adam Salamba aliyefunga dakika ya 22 baada ya kumpiga chenga mlinzi wa Pachoto Stars FC, Abdulrahman Masimika na kupiga shuti la juu lililomshinda mlinda mlango wao, Fadhil Ussi.
Mchezo uliohusisha baina ya timu ya Navy FC na Kariakoo ulimalizika kwa sare tasa ya 0-0 ikiwa Karikoo ikiendelea kusuasua kwa kulazimishwa sare ya pili katika ligi hiyo.
Klabu za Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma na Bulyanhulu FC ya Shinyanga zimeanza kuonyesha dhamila ya kupigana vikumbo vikali vya kugombea nafasi ya kwanza ili kituo cha Morogoro katika ligi ya mabingwa ya mikoa kwa kukusanya pointi saba katika mngwe ya kwanza mkoani hapa.

0 comments:
Post a Comment