BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK BILAL AHANI MSIBA WA MKE WA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji katika msiba wa mke wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelil, wakati alipofika kumfariji Katibu huyo nyumbani kwake Boko Jijini Dar es Salaam, jana jioni. Mazishi yanatarajia kufanyika leo jioni kwenye Makaburi ya Kinondoni.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Adama Malima, akizungumza machache katika shughuli hiyo ya kuhani msiba huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha mke wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelil, wakati alipofika kumfariji Katibu huyo nyumbani kwake Boko Jijini Dar es Salaam, jana jioni. Mazishi yanatarajia kufanyika leo jioni kwenye Makaburi ya Kinondoni.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: