BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KATIKA HILO GROGBA ATAKUMBWA MILELE NA MILELE NCHINI UTURUKI

 
Mshambuliaji wa Galatasaray Didier Drogba amefanya kitendo ambacho kimezidi kumpa sifa kubwa pindi linapokuja suala la kurudisha kwa jamii. Drogba ambaye alitangaza rasmi kuondoka Galatasary baada ya mkataba wake wa miezi 18, ametoa mchango wa €1 million ambazo ni zaidi ya billioni na nusu za kitanzania kwa familia za wahanga wa maafa yaliyotokea kwenye machimbo ya madini nchini Uturuki.

Drogba na wachezaji wenzie wa Galatasary walivaa ‘helmets’ kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuonyesha sapoti juu ya tukio lilotokea machimboni, lakini muivory coast akachukua hatua nyingine ya ziada kuwasaidia wahanga wa maafa akiwa kama balozi wa Umoja wa Mataifa.

“Mimi ni balozi wa U.N na nitafanya kila kitu kusaidia watu waliopata maafa kule Soma,” Drogba aliwaambia waandishi wa habari.

“Lakini sihitaji mtu yoyote atumie jina langu kujipatia umaarufu kupitia janga hili, mimi sio mtu wa kujipromoti kwenye vitu kama hivi.”

Tarehe 13 mwezi huu kwenye migodi ya makaa kulitokea mlipuko mkubwa uliosababisha vifo vya watu 301.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: