BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KINACHOWAKUTA YANGA SASA HIVI NI HIKI, BAADA YA KAVUMBAGO NA DOMAYO KUTIMKA AZAM FC, HUYO NDIYE ANAYEFUATIA.

Kocha wa timu ya yanga Hans Van Der Pluijm.

Kocha wa yanga ya Tanzania Yanga, Hans Van Der Pluijm anetangaza rasmi kujiondoa katika timu hiyo na kujiunga na timu mpya ya nchini sadi Arabia baada ya mkataba wake wa miezi sita aliosaini ndani ya timu hiyo kumalizika.
Akizungumza na wanahabari muda mfupi uliopita ndani ya makao makuu ya timu hiyo kocha huyo amesema kuwa makubaliano yake na timu ya yanga yalikuwa kuifundisha ndani ya miezi sita na baada ya hapo atajiunga na timu yake mpya ambayo ipo ndani ya moyo wake ya nchini saud Arabia.

Pamoja na kuondoka kwake kocha HANS amewaahidi viongozi wa yanga kuwa atawasaidia kwa kuwaletea wachazaji wawili kutoka nchini Ghana ambao wataisaidia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu nchini Tanzania.

Aidha amesema kuwa atakuwa nchini Saudi Arabia kwa mwaka mmoja huku akisema kuwa kama yanga inamtaka baada ya hapo yupo tayari kurejea tena nchini kuifundisha tena club hiyo kwani ndio kazi yake.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: