MATUKIO YA AFRIKA.
Mbabe wa kivita wa DRC Germain Katanga akiwa mjini The Hague.
Mahakana ya Kimataifa ya Uhalifu ya mjini The Hague
Uholanzi imemuhukumu mbambe wa kivita kutoka Congo, Germain Katanga,
miaka 12 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuwapa silaha kundi la
waasi 2003 na kufanya mauwaji.
"Mahakama imemuhukumu Germain Katanga kifungo cha miaka 12 gerezani," alisema Jaji Mkuu Bruno Cotte mbele ya mahakama ya The Hague ikiwa ni hukumu yake ya pili tangu kufunguliwa kwake mwaka 2003. Jaji huyo amesema kile kipindi cha miaka saba ambacho mtuhumiwa amekutimia akiwa kizuizini kitapunguzwa katika miaka ya kifungo chake.
Mwezi Machi mwaka huu, Katanga mwenye umri wa miaka 36, alikutwa na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu, yakiwemo mauwaji na uporaji kutokana na jukumu lake katika harakati za kuvamia kijiji cha Bogoro katika eneo tete la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 24 Februari 2003.
Dhati ya hukumu
Makauburi waliozikwa waliouwawa Ituri
Wakati ikitangazwa hukumu hiyo, Katanga ambaye anajulikana kwa jina la utani la Simba, hakuonesha mtikisiko wowote mahakamani hapo. Inaelezwa kuwa matukio hayo ya uhalifu yalifanyika wakati akiwa na umri wa miaka 24.
Jaji aligundua kuwa alilipa silaha kundi la wapiganaji la Patriotic Resistance Forces la mjini Ituri (FRPI) ambalo liliuwa idadi kubwa ya watu, ikikadiriwa kuzidi 200. Jaji Cotte ameiambia mahakama ya ICC kwamba makovu ya mapigano ya Februari 24, 2003 yameendelea kuonekana mpaka leo hii. Amesema kutumika kwa mapanga katika mashambulizia hayo ilikuwa vitendo vya kikatali sana na kwamba kumesababisha maumivu yaliyokithiri.
Kupunguzwa kwa mashitaka
Hata hivyo, awali mahaka ya uhalifu wa kivita ICC ilimfutia mashitaka Katanga ya ubakaji, utumwa wa kingongo, na kutumia watoto wenye umri mdogo jeshini. Baada ya kutolewa hukumu hiyo wanasheria kutoka kwa upande wa Katanga watakuwa na siku 30 ya kukataa rufaa kufuatia hatua hiyo. Hata hivyo uhamuzi rufaa hiyo bado haujatolewa.
Hukumu hio ni ya pili kutolewa tangu kufunguliwa milango ya mahakama hiyo mwaka 2003, nyingine ilikuwa ya mbambe wa kivita ambae kwa wakati fulani alikuwa hasimu wake Thomas Lubanga ambae mwaka Julai 2012 alihukumiwa miaka 14 gerezani.
Hukumu ya funzo kwa waharifu.
Kufuatia hukumu hiyo mmoja kati ya wanahakaraki wa haki za binaadamu kutoka katika umoja unaoshiorikiana na mahaka ICC ili iweze kutekeleza majukumu yake Joseph Dunia Luyenzi amesema inatoa matumaini kwa waathirika na kupeleka salamu kwa wale wote wanaotenda uhalifu kuwa watakuwa wakifuatilia na sheria kuchukua mkondo wake.
Hukumu ya mtuhumiwa huyo ilikuwa tata baada ya mmoja kati ya majaji watatu katika keshi hiyo kusema uamuzi wa kubadili muundo wa awali wa kesi hiyo utaathiri uwezo wa kujitetea. Awali Katanga alishitakiwa kama mshiriki mwenza asiekuwa wa moja kwa moja na kufanya kuwa mwezeshaji katika uhalifu huo. Hatua hiyo imeshusha kiwango cha ushiriki wake katika shambulio hilo la kijiji cha Bogoro.DW
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / THE HAGUE YAMHUKUMU MBABE WA KIVITA WA DRC CONGO GERMAIN KATANGA MIAKA 12 GEREZANI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment