BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAANDISHI WA HABARI MOROGORO NAMNA WALIVYOADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KILOSA-MOROGORO.

Waandishi wa habari wakiwa katika maandamano huku wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti wakipita eneo la stendi kuu wakati wa maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (Moro Press Club) yaliyoadhimishwa katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
 
Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communication Ltd Morogoro, Lilian Lucas kushoto akimjulia hali Safina Saidi (34) mkazi wa Kilosa mjini aliyejifungua watoto mapacha katika wodi no 1 ya hospitali ya wilaya ya hiyo baada ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa wakati wa maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (Moro Press Club) wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Katibu Mtendaji wa Morogoro Press Club, Abeid Dogoli kulia na Kutty Libenanga wakimkabidhi sehemu ya msaada Kaimu Mganga wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kuwakabidhi wagonjwa.
Wanachama wa Morogoro Press Club wakiwa na vipande vya sabuni kwa ajili ya kutoa msaada kwa wagonjwa hospitali ya wilaya ya Kilosa.
Katibu Mtendaji wa Morogoro Press Club, Abeid Dogoli akitoa msaada wa sabuni kwa bibi ambaye alikuwa anauguza mjukuu wake.
Mratibu wa Morogoro Press Club, Thadei Hafigwa akitoa msaada kwa mama mjamzito katika wodi namba moja ya wazazi.
Mratibu wa Morogoro Press Club, Thadei Hafigwa akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Safu ya viongozi wa meza kuu na waandishi wengine (hawapo pichani) wakiomba dua kwa Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Morogoro, Venance George aliyefariki dunia hivi karibuni kabla ya kuanza kwa mdahalo uliowakutanisha wadau mbalimbali wa habari wilayani Kilosa.
Sehemu ya waandishi wa habari wakiongozwa na Mkuu wa waandishi wa gazeti la Majira Morogoro, Aziz Msuya (aliyekunja nne) wakati wa maadhimisho hayo.


Lilian Justice wa gazeti la majira na mpiga picha wa ATV Athumani Shekiondo kushoto wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika ukumbi wa Babylon Kilosa.


Katibu Mkuu Mtendaji wa chama Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (Moro Press Club) Abeid Dogoli akitelemka katika gari la wagonjwa la hospitali ya wilaya ya Kilosa mara baada ya kuliendesha kutokanan na utata uliogubikwa kuwa gari hilo ni bovu wakati waandishi walipotembea hopsitali kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Morogoro juzi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: