BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BRAZIL WAANZA KWA KUSHINDI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA CROTIA.

20140613-010343-3823241.jpgHatimaye baada ya subira ya miaka minne, wapenzi wa soka ulimwenguni kote leo wamepata ladha ya fainali za michuano ya kombe la dunia.


Mchezo wa ufunguzi ulichezwa leo baina ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia, matokeo ni 3-1, Brazil wakianza vizuri michuano hiyo mbele ya Croatia.

Magoli ya Brazil yamefungwa na Neymar, aliyefunga mawili, Oscar nae ambaye jana alikuwa kwenye kiwango bora aliongeza la 3.

Croatia wenyewe walianza kuziona nyavu zao kwenye mchezo huo walipata goli lao mapema kabisa ya mchezo baaada ya beki wa Brazil Marcelo kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa.


Michuano hiyo itaendelea tena leo saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kati ya Mexico dhidi ya wawakilishi wa Afrika Cameroon.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: