Brazil imeponea kung'olewa kutoka mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini humo.
Hii ni baada ya mechi ya kwanza ya mkondo wa muondoano kati yake na Chile kumalizika kwa mikwaju ya Penalti baada ya timu hizo mbili kwenda sare ya bao moja baada ya kipindi kizima cha mechi.
Na pia baada ya kucheza muda wa ziada.
Wakati wa mikwaju ya Penalti, Brazil iliingiza tatu huku Chile ikiingiza mbili.
Wakati wa mechi, Brazil iliingiza bao la kwanza la mechi ndani ya kipindi cha kwanza, lakini Chile ilileta jibu kabla ya kipindi cha kwanza cha mechi kukamilika.
Brazil ilikuwa na kibarua kigumu na shinikizo tele kutoka kwa mashabiki wa Brazil ambao walijaa uwanjani na pia kwa kuwa Brazil ni mwenyeji wa michuano hiyo, matarajio ya wengi nchini Brazil ni kuwa wanatafanya vyema katika mashindano hayo.
COLOMBIA 2-0 URUGUAY.
Timu mbili zimeendelea mbele kwenye robo fainali baada ya mechi za leo kufanyika. Brazil baada ya kushinda ushindi wa penati imekua timu ya kwanza kwenda kwenye robo fainali. Colombia nao wamewafunga Uruguay magoli 2 – 0 na kuwa timu ya pili kwenda robo fainali.
0 comments:
Post a Comment