BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MANZESE MTAA HATARI ZAIDI KWA UHARIFU MOROGORO.

Askari kanzu wakimdhibiti mmoja wa vijana wanaojihusisha na uharifu wa kutumia simu sababu baada ya kumkamata eneo la Sabasaba Manispaa ya Morogoro hivi karibuni.

 
Miongoni mwa mitaa ya Manispaa ya Morogoro inayoogopeka na kuvuma kwa sifa mbaya ikiwemo baadhi ya sehemu ya vijana kujiingiza katika matukio ya uharifu kwa kujihusisha kupora mali kwa watu wanaopita mitaa ama kutembelea ndugu na jamaa basi huwezi kukosa kuutaja Mtaa wa Manzese uliopo katika Kata ya Mafiga kwa sasa.



Mtaa wa Manzese una sifa ya baadhi ya vijana wake kujihusisha kwenye matukio ya uhalifu wa mali za watu kwa rika tofauti kwa kupora mikoba, simu, fedha nakadhalika.



Watu huporwa mali hizo kwa nyakati za asubuhi, mchana, usiku na alfajiri ambapo vijana hao hukuba na kuiba kwa mfumo wa karata tatu, kusachi kwenye mifuko ya suluari na mikoba na wizi wa kuuza simu kanyaboya maarufu simu sabani.

SABUNI YENYE UMBO LA SIMU AMBAYO HUWEKWA KATIKA BAHASHA YA KAKI NA KUUZIWA MTU BAADA YA KUONYESHWA SIMU HALISI.


Mkazi wa mtaa huo mwenye cheo ndani ya serikali ya mtaa ambaye jina lake hakutaka kuchapishwa kwa kuhofia usalama wake anafichua tabia za ukatili zinazofanywa na vijana hao na watu wanaowaficha wahalifu kwa manufaa yao hasa ya kununua mali zinazoibwa na kuporwa na wahalifu hao kutoka kwa watu mbalimbali ndani ya Manispaa ya Morogoro.



Alieleza hayo katika mahojiano maalum na mwandishi wa makala haya ya uchunguzi juu ya vitendo hivyo vinavyosababisha mtaa huo kuogopwa mchana na usiku.


“Ni kweli huu Mtaa wa Manzese umekuwa na matukio ya kikatili kwa watu wanaotembelea ndugu zao ama kupita kwenda sehemu nyingine. Watu wanakumbana na adha ya kuporwa mali zao na wakati mwingine mtu ataambulia kipigo na kujeruhiwa,”alisema kiongozi huyo.


Alisema ilifika wakati viongozi wa ngazi ya mtaa walifikia hatua ya kuomba msaada kwa Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha Mzinga ili kupunguza kasi ya vijana hao.



“Mimi nina ushahidi na nimeletewa kesi nyingi tu za watu kuporwa mali huku mikono ikivuja damu baada ya kuporwa na kupigwa lakini ninapopeleka suala katika vyombo vya dola usishirikiano unakuwa mdogo. Mhalifu akikamatwa siku hiyo hiyo anarudi mtaani na kuendelea na kazi hiyo ya kukaba na kupora mali.”alisema.



Vijana hao wanadaiwa kutoka katika kata za Mjimpya, Mifusini-Mafiga na Chamwino ambapo nyakati za ashubuhi, mchana na jioni huendesha shughuli za uhalifu eneo la Manzese kabla ya kuhamia sehemu nyingine nyakati za usiku mnene.


Alisema sehemu kubwa ya matukio yameripotiwa katika kituo cha polisi lakini askari polisi ngazi ya wilaya hawatoi ushirikiano na badala yake wamekuwa wakidai rb huku baadhi ya askari wakichukua pesa kutoka kwa watuhumiwa na kuachia huru, jambo ambalo lilisababisha viongozi kwenda katika kambi ya Mzinga kuomba msaada wa askari jeshi.



“Kimsingi matukio haya yanachangiwa na baadhi ya askari wasiowaaminifu na kulitia aibu ambao wamekuwa karibu na wahalifu ambao bila aibu huchukua fedha siku za Jumamosi na Jumapili katika minada ya Kikundi na Sabasaba baada ya kuwapora watu katika minada hiyo.”aliongeza.



Maeneo ambayo ni hatari kwa uporaji ni Barabara ya Sabasaba, Kanisa la Anglikana, Peoples Park na Stendi ya Melela ambako vijana hao husimama kando ya barabara,’’alisema Nassour Makumvi.



Makumvi alisema wezi wamegawanyika katika makundi manne, yaani wizi wa fedha kwa njia ya kusachi mifukoni na mikoba kwa kutumia wembe, wizi wa simu sabuni, karata tatu na ule wa kukaba nyakati za giza ikiwa imeingia.



Mkazi huyo ambaye ni miongoni mwa wakazi wanaoendesha shughuli zao katika maeneo hayo alisema vijana hao wana umoja wa hali ya juu na kwamba endapo utawaingilia katika kazi yao utakuwa katika hatari ya kudhurika.


Kama ndugu yako ameibiwa na vijana hao kinachofanyika ni kuwafuata kwa upole na kuomba kurejesha kile walichopora iwe simu au begi lakini sio vinginevyo.


Kuna dhana ambayo tayari imejengeka kuwa baada ya vijana hao kufanya tukio na wale wanaofanikiwa kupelekwa kituo kidogo cha Polisi cha Kingo huachiwa baada ya dakika 10 na kurejea tena eneo hilo kutenda uhalifu.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Kenyatta katika Kata ya Sabasaba, Robert Mkasanga anasema kuna zaidi ya vijana 25 wanaotoka katika Kata ya Mafiga wanaofanya uhalifu wa kupora wapitia njia.

Mwaka 2011 kasi ya uhalifu ilipungua kwa kiasi kikubwa baada ya uongozi wa jeshi la polisi kipindi hicho kukomesha vitendo hivyo katika eneo hilo lakini sasa wamerejea tena kwa kasi.



Katika mchezo wa karata tatu wamekuwa wakiwatumia wanawake kama chambo kwa wanawake wenzao na vijana wanaopita maeneo yanayochezwa mchezo huo hukumbwa na adha hiyo ya kulazimishwa kucheza na kama hatakuwa tayari basi itatumika nguvu ya kumpora mali kilazima.


Mkasanga alisema kuna mnunuzi maalum wa mali zinazoporwa na vijana hao kutoka kwa watu mbalimbali waliokumbwa na mkasa huo.

KIJANA AKIMSHAWISHI MPITA NJIA SIMU HALISI ILI AINGIE KANYABOA NA KUMBADILISHIA SABUNI YENYE UMBO LA SIMU.


Uongozi wa jeshi la polisi kwa kutosikiliza malalamiko ya viongozi wa mitaa hasa kuhusu kero hiyo ndiyo tatizo linalowapa kiburi wahalifu hao.


“Haiwezekani kiongozi wa polisi ngazi ya wilaya umpe taarifa ya uhalifu halafu anakujibu anavyojisikia yeye sasa hapo mtoa taarifa unataka atafsiri nini juu ya wahalifu hao na viongozi?.”alihoji Mkasanga.


Aliongeza kuwa kwa mfumo huo wa kufumbia macho ndiyo uliosababisha hata milango ya kituo kidogo cha polisi Kingo kata ya Sabasaba kung’olewa na kuibiwa na wezi hao na hapo ndipo inapotoa picha halisi ya uhalifu wa vijana hao na kama wanadhubutu kuiba milango tena kituo cha polisi nini unategemea kwani bila shaka hilo linatoa picha namna matukio ya uhalifu yalivyo.



Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo alisema kuwa vijana hao wamegawanya masaa ya kufanya kazi yao hiyo haramu huku wakiwa na vitendea kazi kama viwembe, visu, nondo, mapanga ambapo pindi wanapomvamia mtu humlazimisha kwanza kutoa pesa na kukiwa na kauli ya kupishia kile wanachotaka wao basi watamjeruhi kwa silaha hizo.


“Natenganishwa na barabara tu lakini kazi zao nyingi hufanyia upande wa mtaa ninaouongoza lakini sikubaliani na vitendo vyao na nimekuwa mkazi na wakati mungine najikuta naelemewa huku nikilazimika kujiwekea ulinzi kwa kuajiri walinzi wawili wa kulinda mali zangu nyakati za usiku kwani vitisho wanavyotoa sio vya kupuuzia.”alisema Mkasanga.


Mwandishi wa makala hayo ambaye alifanya uchunguzi wa kina takribani mwezi moja alibaini kuwepo kwa matukio hayo na kushuhudia baadhi ya matukio ya uhalifu wa njia ya uporaji, wizi wa kusachi fedha mifukoni na katika mabegi, michezo ya karata tatu katika eneo hilo na kulazimika kuonana na kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi LeonardPaulo ili kuona ukweli wa tukio hilo.


Baada ya mwandishi kufika ofisi ya kamanda na kumweleza juu ya malalamiko ya wananchi na baadhi ya askari wake kushindwa kudhibiti na komesha uhalifu katika mtaa huo wa Manzese unaofanywa na vijana kwa kupora mali za watembelea kwa miguu.


Kamanda:swali lako mwandishi siwezi kukupatia majibu ya moja kwa moja na hii inatokana na yeye kuhamishiwa mkoa wa Morogoro akitokea mkoa wa Geita hivyo apewe muda wa wiki moja na baada ya hapo ndipo mwandishi arejee kuona nini kimefanyika katika kipindi hicho.

Kamanda Paulo aliongeza kwa kusema wiki moja aliyoitoa kwa mwandishi inatosha kwa yeye kujipanga na kukomesha tabia na kuacha mtaa wa Manzese kurejea katika hali ya usalama na watu kuendelea na shughuli zao kama zamani


Akitolea ufafanuzi baada ya wiki moja kupita, Kamanda Paulo alisema kuwa ndani ya kipindi cha wiki moja jeshi hilo tayari imewatia nguvuni wahalifu 11 na kati yao watatu wahalifu sugu waliokuwa wakisakwa kwa udi na ufumba.


“Yes tulifanya operesheni maalum na kukamata wahalifu 11 na watatu kati yao ni wahalifu sugu waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu na hapa ninapoongea na wewe baadhi yao tayari wamehukumiwa kifungo jela kutokana na makosa mbalimbali walioyatendaya kiuhalifu.”alisema Paulo.


Aliongeza kwa kusema kuwa ili jeshi la polisi liweze kufanya kazi yake vizuri ni lazima kuwe na watu waliotayari kufichua maovu kwani tunahitaji watu wenye moyo wa uzalando nami huu mkoa ni bado ni mgeni na cha msingi nahitaji ushirikiano na sio mgeni katika kazi laa, ni ugeni wa kusoma mazingira ya kuhufahamu huu mjini na tutaendelea kuufuatilia usalama wa mtaa wa Manzese kwa ukaribu zaidi ikiwemo na mitaa mingine.”alisema Paulo.


Kitu cha msingi katika kukomesha uharifu katika mitaa ya Manispaa ya Morogoro na mkoa kwa ujumla ni lazima wananchi wawe tayari kuwafichua waharifu ambao wanaishi nao huko mitaa ili amani kama sera ya jeshi la polisi inavyoeleza kulinda usalama wa raia na mali zake.alisema Kamishna huyo, Paulo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: