Mbunge wa Chalinze, mkoani Pwani, Riwadhani Kikwete, mwishoni mwa wiki aliwafukuza waandishi wa habari kushiriki katika mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro, huku akidai kuwa waandishi wengi wa Tanzania ni makanjanja.
Pia amewataka wasomi kutojiunga na fani hiyo ambayo alisema watu wake waandika vitu vya hovyo hovyo.
“Nyie waandishi sikuja hapa kwa ajili yenu, nimekuja kwa ajili ya hawa wanafunzi, kwa hiyo tegesheni kamera zenu halafu ondokeni, ” ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bagamoyo.
Katika hotuba yake, Ridhiwani alisema waandishi wengi wanasukumwa sana na weledi wa jinsi yeye anavyofikiria kichwani na itikadi ya siasa yake.
“Wakati mwingine hata jambo linapofanyika yeye kusifia hawezi, yeye kazi yake ni kuandika vitu vya ovyo ovyo tu. Niwakumbe juzi tulikuwa tunajadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati. Mambo yaliyofanywa na wizara ile katika kipindi cha mwaka 2014/15 ndugu zanguni mazuri sana, mazuri kweli kweli,” alisema.
Alisema lakini cha ajabu zaidi siku moja kabla ya wabunge kwenda kujadili hotuba hiyo, magazeti yaliandika Waziri Muhongo kikaangoni.
“Kikaongoni hicho kipi, CCM oyee, sasa hayo ndiyo magazeti tuliyonayo, magazeti ambayo yanaandikaandika tu yaani mpaka wakati mwingine mimi nashindwa hata kuelewa maana juzi tulikuwa pale wenye mjadala wa Wizara ya Habari makelele yaakaanza, tunaka mjadala, tunaka waandishi walio huru, tunataka waandishi nini. Mimi nikawanasema moyo kwa jamani hivi tukileta huo mswada wa waandishi wa habari, hao waandishi wa habari kesho hawatalia?” alisema.
Kwa mujibu wa Ridhiwani, hofu yake hiyo inatokana na ukweli kwamba asilimia kubwa ya waandishi wa habari waliopo ni makanjanja tu.
“Ni ukweli kabisa wanapokaa katika meza zao, wanaandika tu vitu, wanapokaa katika ofisi zao wanaandika tu vitu, yaani mtu anapikapika tu vitu. Mimi ningetaka sana kuwasihi waandishi wetu hebu kidogo tuandike vitu vinavyofanana na hali halisi,” alisisiza Ridhiwani.
Alisema rai hiyo haimanishi kwamba watu wanapofanya maovu wanyamaziwe.
“Hapana, wanapofanya maovu yaandikwe mabovu yao, wanapofanya mazuri wasifiwe na ili tuendelee kutiana moyo kutengeneza taifa hili la Watanzania. Watanzania wana mahitaji mengi sana…Amani na utulivu wa mioyo yao,” alisema Ridhiwani.
Alisema mioyo ikishatulia mambo yote yanakwenda vizuri, lakini kama kuna hali ya wasi wasi inayotokana na yanayoandikwa kwenye magazeti hakuna uhakika kama kesho Rwanda na Tanzania hazitaanza vita.
Alisema hali hiyo inaweza kuwafanya watu wa mipakani watamani kukimbilia ama Morogoro au Dar es Salaam wakiamini kuwa ni mbali, jambo ambalo si haki.
Ridhiwani aliwataka wasomi hao wasiingie kada hiyo na wasikumbwe na ushabiki wa kisiasa na badala yake waipende sana nchi yao.
VIDEO YA KAULI HIYO YA RIDHIWANI DHIDI YA WAANDISHI ITAWAJIA MARA BAADA YA KUIANDAA.
VIDEO YA KAULI HIYO YA RIDHIWANI DHIDI YA WAANDISHI ITAWAJIA MARA BAADA YA KUIANDAA.

0 comments:
Post a Comment