
Nahodha wa timu ya Schalka 04 ya Dodoma Mussa Gaidi akiwa na wachezaji wenzake wakifurahi kutwaa ubingwa wa kanda ya Kati wa mashindano ya Castle Lager Perfect Six baada ya kushika nafasi ya kwanza kutoka kanda ya Kati katika michezo iliyofanyika uwanja wa Fire manispaa ya Morogoro kwa kukusanya pointi tisa ambapo itawakilisha michezo ya ngazi ya taifa kuwania safari ya kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona.PICHA/MTANDA BLOG.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Mashariki, Julius Nyaga kushoto akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Schalke 04 ya Dodoma, Mussa Gaidi baada ya timu yake kushika nafasi ya kwanza ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya Kati katika michezo iliyofanyika uwanja wa Fire Morogoro kwa kukusanya pointi tisa ambapo itawakilisha kanda kwenye ngazi ya taifa kuwania safari ya kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona. PICHA/MTANDA BLOG.


Mshabuliaji Ibrahim Nyagawa (Chuji) wa Schalke 04 ya Dodoma akikokota mpira wakati wa fainali za Kanda ya Kati hizo Morogoro

ssa Kandula wa Mzinga FC na Delta Thomas wa Ndezi FC wakipambana kwenye fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya ya kati huko Morogoro.
Na Mtanda Blog, Morogoro.
Timu ya soka ya Schalk 04 ya Dodoma imetwaa ubingwa wa mashindano mapya ya Castle lager Perffect 6 mwaka 2014 kanda ya mashariki baada ya kuongoza na kushika nafasi ya kwanza katika michezo ya ligi ndogo ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Ubingwa huo kwa timu ya Schalk 04 inatoa nafasi ya kuwa mwakilishi kutoka kanda ya mashariki kugombea nafasi ya kwenda nchini Hispania kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona katika la liga endapo itashika nafasi ya kwanza katika michezo ya fainali ya ngazi ya taifa ya mashindano hayo yatayofanyika jijini Dar es Salaam siku za baadaye baada ya kupata mabingwa kutoka kanda nane.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mjini Morogoro, Meneja wa Bia ya Castle, Kabula Nshimo alisema kuwa katika michezo ya ligi ndogo ya kanda ya mashiriki ilikuwa na ushindani mkali kutokana na kila timu kujiandaa kushinda na kuibuka mabingwa katika kanda hiyo ambapoSchalk 04 ndiyo mabingwa wa kihistoria katika kanda ya mashariki 2014.
Nshimo alisema kuwa schalk 04 ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa kushinda michezo yake mitatu na kujikusanyia pointi tisa huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mzinga FC ya Morogoro iliyopata pointi sita wakati Ndezi FC ya Morogoro imekusanya pointi tatu na kushika nafasi ya tatu na Market FC ya Dodoma ikiishia kupoteza michezo yote.
“Haya mashindano ya Castle lager perffect 6 ni mashindano mapya hapa Tanzania lakini endapo timu zetu kuanzia zile za ligi ya ngazi ya wilaya, mikoa, ligi daraja la kwanza na ligi kuu ya vodacom zikiiga mfumo wa uchezaji wake zitakuwa timu za kutoa upinzani na zitafanya vizuri kwani timu zinazoshiriki zinafuata uchezaji wa mfumo wa klabu ya barcelona ya Hispania kwani hao ndiyo wanaosifika kwa kutandanda soka safi.”alisema Nshimo.
Barcelona inasifika kwa wachezaji wake kupasiana pasi fupi fupi na kumfikia mlengwa na endapo timu za Tanzania zitaiga mfumo huo itasaidia Tanzania kupata timu ya taifa yenye kutoa ushindani mkubwa katika michezo ya kimataifa na kufuzu katika michezo ya kombe la dunia ikiwemo na bara la afrika.aliongeza Nshimo.

0 comments:
Post a Comment