BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU NANE WAPOTEZA MAISHA KWA KUUMWA NA MBWA MJINI SONGEA MKOA WA RUVUMA.


Watu nane wamefariki dunia kwa kuumwa na mbwa wenye kichaa wilayani songea mkoani ruvuma.

kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu watu wa nane wamefariki dunia kwa kuumwa na mbwa wenye kichaa.
 
Huku manispaa ya songea inayotikiswa kwa ugonjwa huo ikiwa haina dawa za kutibu watu walioumwa na mbwa kichaa na pia idara yake ya mifugo haina pesa za mafuta kuzungukia kuua mbwa wenye kichaa.

 
Taarifa hiyo imetolewa na kaimu afisa mifugo wa manispaa ya songea mkoani Ruvuma Gaspar Tillya na kwamba kutoka na hali hiyo msako mkali umekuwa ukiendeshwa wa kuwasaka mbwa wenye kichaa ingawa unakwazwa na ukosefu wa pesa  huku wanajeshi wakisaidia kusaka mbwa hao kutokana na baadhi ya mbwa hao kuingia kwenye kambi ya jeshi ya chandamali ya mjini songea.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: