BOKO HARAM YAILAZIMISHA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MAGARI KWA SIKU TATU MFULULIZO NCHINI NIGERIA.
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati wa siku kuu ya Eid ul Fitr.
Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.
Kundi la Boko Haram limetishia kulipua bomu la gari
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri waislamu kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi katika viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.
Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka bendera zake.
Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao.BBC
0 comments:
Post a Comment