DAKTARI AAMBUKIZWA VIRUSI VYA UGONJWA WA EBOLA WAKATI AKIWATIBU WAGONJWA WALIOATHIRIKA NA EBORA.
Wafanyakazi wa afya wakielimisha umma juu ya ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi.
Dr. Umar Khan anasifiwa na wananchi wa Sierra Leone kama shujaa aliyejitolea kusaidia waathirwa wa Ebola.
Daktari mwenye umri wa miaka 39 anayeongoza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola huko Sierra Leonne ameambukizwa ugonjwa huo mwenyewe.
Wizara ya afya nchini humo inasema Dr.Umar Khan amepelekwa kwenye eneo la matibabu ambalo linaendeshwa na madaktari wasio na mipaka - (Doctors Without Borders).
Habari za kuambukizwa kwake zilitangazwa Jumatano baada ya wauguzi watatu katika kituo hicho cha Kenema kufariki kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Dr. Umar Khan anayelezwa kuwa shujaa huko Sierra Leone. Eneo la Kenema lipo kilometa 300 mashariki mwa mji mkuu Freetown.
0 comments:
Post a Comment