Kituo cha mafunzo ya watoto maarufu kama jela ya watoto jijini Tanga, inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo ukosefu wa chakula na huduma ya maji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Akizungumza na NIPASHE mjini hapa jana, Mkuu wa kituo hicho ambaye pia ni Afisa Ustawi wa Jamii, Clara Kibanga, alisema kituo hicho ambao kwa sasa kina watoto tisa, wawili wa kike na saba wa kiume, wamekuwa wakiishi kwa kutegemea wahisani ambao nao hujitokeza kutoa misaada mara moja moja.
Kibanga alisema kwa takribani mwezi mmoja sasa kituo hicho hakina huduma ya maji kutokana na kukatiwa kwa kushindwa kulipa ankara hatua ambayo inawalazimu kuomba maji kwa majirani wanaoishi karibu na eneo hilo jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watoto hao.
“Kituo kina watumishi sita tu, kati yao wawili ni walinzi na watoto hawa wamewekwa hapa kutokana na makosa mbalimbali sasa tunapoanza kujichanganya na kuomba maji kwenye nyumba za raia nje ni hatari sana kwa maisha ya hawa watoto lakini chakula nacho ni tatizo sana”, alisema Afisa huyo.
Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa samani kama viti na meza, ukosefu wa uzio pamoja na uchakavu wa majengo na miundombinu ya maji safi na majitaka.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendegu, alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya jiji hilo, Juliana Mallange, kuhakikisha wanalipa ankara ya maji mara moja ili kurudisha huduma hiyo muhimu kituoni hapo.
“Mengine yapo chini ya wizara na mengine yapo chini ya halmashauri sasa ni vema DED akashughulikia suala la maji mara moja ili kurudisha huduma kituoni, lakini hili samani mimi mwenyewe nitatoa meza 10 na viti 10”, alisema Dendego.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya alikabidhi zawadi za Eid el Fitri kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambazo ni mbuzi wawili na mchele kilo 100. CHANZO: NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment