BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NAPE NNAUYE AKIMKEJERI DK SLAA KATIBA MPYA.


http://pamelamollel.files.wordpress.com/2013/11/47172-3b-napeakihutubiamaelfuyawananchiuwanjawashuleyamwakatunduma.jpgCHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kitazungumzia mambo mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye Kamati Kuu ya CCM likiwamo suala la mgombea urais kupitia chama hicho. Hivi karibuni baadhi ya wanachama wa chama hicho kwa nyakati tofauti wameweka hadharani nia ya kuwania nafasi ya urais ndani ya CCM.

Miongoni mwao ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye tamko lake la nia ya kugombea, lilizua mjadala katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Akijibu swali la waandishi wa habari jana waliotaka kufahamu kama Kamati Kuu ya CCM imejadili suala la wanachama wanaotangaza nia, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema,“suala la mgombea urais ni moja ya mambo ambayo kesho (leo) nitazungumza nanyi (waandishi).”

Akizungumzia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), Dk Willibrod Slaa ya kuwapo waraka maalumu wa mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba, Nape alisema taarifa hizo ni uzushi mtupu.

“Taarifa za kuwapo waraka maalumu kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba ni uzushi mtupu na unadhihirisha namna walivyo wavivu wa kufikiri kiasi cha kutunga andiko na kutangaza wenyewe,” alisema.

Slaa alinukuliwa na vyombo vya habari akidai kuwapo kwa waraka maalumu wa CCM ulioandaliwa na Kamati maalumu na kuuwasilisha kwa katibu mkuu ili aupeleke kwa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, ikiwa ni taarifa ya mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba.

Nape alisema CCM haina haja ya kuhofia mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu ulianzishwa na mwenyekiti wa chama hicho akijua umuhimu wa katiba kwa wakati wa sasa, hasa ikizingatiwa kwamba katiba ya sasa imelifikisha taifa mahali pa kuridhisha kwa miaka 50 iliyopita.

“Watanzania wanatakiwa kutokubali upotoshaji na uzushi wa baadhi ya viongozi na badala yake wajikite katika kufuatilia na kushiriki katika awamu mbili zilizobaki ili kukamisha mchakato wa katiba mpya bila matatizo.”

Kuhusu uhusiano wa CCM na Taasisi ya FriederichHerbert Stiftung (FES), Nape alisema taasisi hizo zimekuwa na uhusiano karibu kwa miaka mingi kutokana na uhusiano kati ya rais wa zamani wa Ujerumani na Baba wa Taifa Julius Nyerere na ni tofauti na Slaa alivyotaka ieleweke kwa jamii.

Wakati huo huo, Nape alisema Kamati Kuu ya CCM imemteua Philip Mangula kuongoza Kamati Maalumu ya wataalamu watakaokuja na tamko (ilani ya 2014/19) ambalo litazungumzia ahadi za chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Mangula pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara.

“Wataalamu hawa watakutana ili kuja na tamko ambalo litakuwa ni ilani kwa chama ambao itakuwa ni ahadi za chama kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa miaka mitano ijayo,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kamati Kuu ya CCM imemteua Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Uhuru Media Group, ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Radio Uhuru.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: