Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia katika mkutano huo.
TAFRANI: ZIARA YA WAZIRI Wanachama wa CCM na Chadema wakizozana katika eneo la Mavurunza, Dar es Salaam jana wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kukagua miradi mbalimbali ya maji kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Picha na Rafael Lubava.
Poilisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada hani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushotona Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru polisikuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza Utakelezaji wa Ilani ya CCM JUU YA MAJI, HUKU mNYIKA AKITAKA WAENDEE KUZOMEA AKIDAI KWAMBA WAZIRI HAKUFANYA HAKI KWANI YEYE ALIPOKUWA AKIZOMEWA NA WANA CCM HAKUWACHUKULIA HATUA KAMA HIYO KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA SHULE YA MAVURUNZA, KATA YA SALANGA
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana.
Mfuasi wa CCM akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, EvaSinare (katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla 9kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.
Mfuasi wa Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali
Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema
Mbunge wa Jimbola Kinondoni, Idd Azzan akihutubia katika mkutano huo
Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambapo aliwahakikishia wananchi wa jiji la Dares Salaam kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia hasa baada ya kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao ujenzi wake umeanza sasa.
Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam na Pwani.
Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutanouliofanyika Kata ya Kibamba.
Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo
Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Taka Dares Salaam, (Dawasco), Jackson Midalla akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata ya Kibamba, Issa Mtemvu wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa maji katika kata hiyo.
Wafuasi wa CCM na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao wakiwakwenye magari eneo la Kibamba. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
HABARI KAMILI.
Dar es Salaam.
Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla jana iliingia dosari baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota (Chadema), kurushiana matusi mbele ya wananchi na nusura wakunjane mashati.
Dar es Salaam.
Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla jana iliingia dosari baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota (Chadema), kurushiana matusi mbele ya wananchi na nusura wakunjane mashati.
Tukio hilo lilitokea jana wakati wa mkutano wa
wananchi wa Kata ya Saranga, Kimara uliofanyika Uwanja wa Shule ya
Sekondari ya Mavurunza ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Makalla katika
ukaguzi wa miradi maji ya Dawasco.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Makalla kuagiza
polisi kuwakamata wafuasi wa Chadema kwa madai kuwa walitaka kuvuruga
mkutano huo. Baada ya Makalla kutoa agizo hilo, Diwani Manota na Mbunge
wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika walisimama na kupinga uamuzi huo na
walirushiana maneno na Mwenyekiti Madenge aliyesema wawili hao waache
upumbavu.
“Unatetea nini? Acha upumbavu... Hatuwezi
kuendesha mkutano na watu wanaofanya vurugu,” alitusi Madenge huku
Manota akiwa na jazba kabla ya viongozi wengine wa kisiasa kuwatuliza.
Hata hivyo, kabla ya Makala kuzungumza, Mnyika
aliyekuwa ameongozana naye katika ziara hiyo alikuwa na wakati mgumu wa
kuzungumza kutokana na zomeazomea kutoka kwa wafuasi wa CCM.
Makalla alisema kosa kubwa lililosababisha kutokea kwa vurugu hizo ni maandalizi mabovu ya wafuasi wa vyama vyote.
“Wafuasi walikuwa na itikadi zao zaidi kuliko kuja
kusikiliza hoja za serikali kupitia ziara. Pia labda waliwakosa
uvumilivu kutokana na ahadi ya maji kuwapo kwa muda mrefu, lakini
kuvurugana wanasiasa ni kukosa uvumilivu,” alisema.
Kwa upande wake, Mnyika alipendekeza ziara zote za kiserikali zisiwe na uhusiano na vyama vya kisiasa.
“Kama ingekuwa ni mambo ya kuzungumzia ilani ya
chama, tangu mwaka 2005/10 ahadi ya maji ya asilimia 90 kwa Jiji la Dar
es Salaam haijatekelezwa,” alisema Mnyika.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment