BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAMILIKI WA BLOG WASHITAKIWA KWA UGAIDI.

 
Wanablogu na wandishi wa Ethiopia walioshitakiwa kwa kosa la ugaidi.

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yameshutumu kukamatwa na kushtakiwa kwa waandishi na wanablogu tisa nchini Ethiopia.

Tume ya Kuwalinda Waandhisi wa habari CPJ, imekosoa serikali ya Ethiopia kwa kutumia sheria ya kukabiliana na ugaidi, kukandamiza harakati zozote za upinzani nchini humo.
Tisa hao walikamatwa mwezi Aprili mwaka huu kwa madai ya kutumia mitandao ya kijamii kuvuruga hali ya asalama nchini Ethiopia.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya Ethiopia, Emmanuel Igunza, anasema kuwa baada ya wanablogu hao kuzuiliwa na polisi kwa zaidi ya miezi miwili na kufikishwa mahakamani mara kadhaa, hatimaye wameshtakiwa na ugaidi.

Tisa hao sasa wanajulikana kama Zone 9 Bloggers.
Viongozi wa mashitaka wamewashutumu wanabulogu hao sita na wanahabari watatu kwa kupokea ufadhili na maagizo kutoka makundi ya kigaidi yanayolenga kuipindua serikali.

Lakini makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamesema mashitaka hayo ni mojawapo ya mbinu za serikali kuzima upinzani na kukandamiza uhuru wa habari.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn awali ameonya kuwa serikali yake haitasita kupambana na yeyote atakayeonekana kuwa na ushirikiano na makundi yaliyopigwa marufuku nchini humo.

Mara kwa mara Ethiopia imeshutumiwa kwa kuwafunga gerezani waandishi wa habari, wanaoonekana kupinga serikali. Wengine wengi wametoroka nchini humo, wakihofia kukamatwa na kuteswa wakiwa jela.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: