Wazazi wa zaidi ya wasichana 200
waliotekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria
wamekataa wito wa kukutana na rais wa taifa hilo Goodluck Jonathan.
Hakuna sababu zozote zilizotolewa na wazazi hao.
Wasichana hao walitekwanyara katika shule yao eneo la Chibok kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Awali shirika la kimataifa la Human Rights Watch lilisema kuwa zaidi ya raia 2,000 wameuawa nchini Nigeria mwaka huu na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Vifo hivyo vinaripotiwa kutokea katika mashambulizi yaliyofanywa katika zaidi ya miji sabini na vijiji Kaskazini mwa Nigeria.
0 comments:
Post a Comment