BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIYEPIGWA WAKATI AKITOKA KUNUNUA BIA BAR APIGA KURA HOSPITALINI YA UAMUZI WA IBARA BUNGE LA KATIBA MPYA DODOMA.


MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka kundi 201, Thomas Mgoli, ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, amelazimika kupiga kura hospitalini, kushiriki kufanya uamuzi wa ibara alizoshiriki kujadili katika Kamati yake.

Akiwa hospitalini hapo, watendaji wa Bunge Maalumu la Katiba walimfuata na kumpa fursa ya kupiga kura kwa utaratibu wa kusema ‘Ndiyo’ au ‘Hapana’, kuhusu ibara 39 iliyopo katika sura ya 4 ya Rasimu ya Katiba mpya, inayozungumzia haki za binadamu, wajibu wa raia na mamlaka za nchi.

Ibara hiyo inataka wananchi wenye ulemavu kuruhusiwa kuingia popote na vifaa vinavyowasaidia, ambayo mjumbe huyo amepiga kura ya ‘Hapana’, akidai kuwa kifungu hicho kinatibua usalama, kwani mlemavu akiruhusiwa kuingia mathalani na magongo, anaweza kuporwa na magongo hayo kutumika kufanya shambulizi.

Alipoulizwa kama afya yake inastahili kupiga kura, alisema alishaandaliwa kisaikolojia na madaktari na kwamba maumivu yaliyopo sasa ya kichwa na shingo, hayawezi kumzuia kufanya uamuzi.

Mgoli alipigwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amewaonya wajumbe wa bunge hilo, kuacha kuhamishia mijadala baa, kwani ni hatari kwa maisha yao.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: