BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DAKTARI MUNGINE WA NIGERIA AAMBUKIZWA VIRUSI VYA EBOLA WAKATI AKIMTIBU MFANYAKAZI WA WIZARA NCHINI LIBERIA.


Daktari aliyemtibu mgonjwa wa Ebola ameabukizwa nchini Nigeria

Daktari mmoja jiji Lagos Nigeria amepatikana ameambukizwa na maradhi ya homa ya Ebola.

Daktari huyo ambaye alimtibu mfanyikazi wa wizara ya hazina nchini Liberia aliyepatikana na homa hiyo ya Ebola na kuwa mtu wa kwanza kuaga dunia nchini Nigeria sasa amedhibitishwa kuambukizwa .

Waziri wa afya nchini humo Onyebuchi Chukwu amesema kuwa daktari huyo pamoja na watu wengine 70 waliokutana na marehemu wametengwa kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Mataifa yaliyoathirika na homa ya Ebola

Patrick Sawyer alitua nchini Nigeria Julai tarehe 20 na akafa tarehe 25 katika hospitali moja mjini Lagos.

Mlipuko huu wa ugonjwa wa ebola katika ukanda wa magharibi mwa Afrika umesababisha vifo vya watu zaidi ya 826 katika mataifa ya Guinea, Liberia na Sierra Leone.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: