BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KINACHOENDELEA KATIKA MAONYESHO YA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI UWANJA WA MWL JULIUS NYERERE NANE NANE MOROGORO.

Afisa wa benki ya NMB Albertina Kanshahu akichua alama za vidole kwa Lucy Kimaro kupitia mashine ya M.Pos wakati wa ufunguaji wa akaunti ya Chap Chap katika banda la benki hiyo katika maonyesho ya wakulima uwanja wa Nane Nane wa Mwalimu Julius Nyerere kanda ya mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOD

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, George Owur akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa benki ya NMB Albertina Kanshahu kushoto namna ya kufungua akaunti Chap Chap inayofunguliwa sehemu yoyote kwa wateja wa benki wakati alipotembelea banda la benki ya NMB Maonyesho ya wakulima kanda ya mashariki uwanja wa Nane Nane wa Mwalimu Julius Nyerere yanayofanyika mkoani Morogoro.CHEZEA NJAA !!! Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoa wa Morogoro, kutoka kushoto Rebeca Nyaulingo-Redio Okoa FM, Remmy Yasinta-TBC, Lilian Justice- Majira, Juma Mtanda, Mwananchi na Hussein Nuha ITV wakipata msosi wa mchana baada ya kuzunguka kwa muda mrefu katika kusaka habari maonyesho ya kimataifa ya wakulima kanda ya mashariki uwanja wa Mwl Julius Nyerere Nane Nane mkoani Morogoro.
Balozi wa Kenye nchini Tanzania George Owur (Mwenye miwani) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa idara ya mimea na vipando katika mazao ya bustani Dk Elias Mgembe wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la chuo kikuu cha kilimo cha Morogoro (SUA) katika maonyesho ya wakulima kanda ya mashariki uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere Nane Nane mkoani Morogoro.Picha/Mtanda Blog.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: