BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBOWE AWAITA WANANCHAMA WA CHEDEMA KUPAMBANA NAYE KATIKA UCHAGUZI WA UENYEKITI.


HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amekubali ombi la Wazee la kumtaka atetea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Septemba 14 mwaka huu.

Licha ya kukubali ombi hilo, Mbowe pia aliwataka wanachama wenye sifa za kugombea nafasi hiyo, kujitokeza kupambana naye, akisema milango ipo wazi kwa yeyote.

Mbowe alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, baada ya kukabidhiwa fomu na Wazee wa chama hicho kutoka mikoa tisa wakimwomba agombee nafasi hiyo tena.

Mbali na Wazee, hafla hiyo pia ilipambwa na wawakilishi wa mabaraza ya Wanawake (Bawacha) na lile la Vijana (Bavicha).

Wazee hao ambao waliongozwa Athuman Mzigo maarufu kama ‘Mapindo Saba’ kutoka Kigoma, pia walikabidhi sh. 50,000 walizojichangisha kwa ajali ya kulipia fomu hiyo.

Kabla ya kukubali ombi hilo, Mbowe alianza kwa kueleza sababu mbalimbali alizodai zimemshangaza kuona ni kwa nini awe yeye licha ya chama kuwa na watu wengi wenye uzoefu na weledi.

Alisema kuwa ameshangazwa na namna makundi mbalimbali yalivyojitokeza na kumtaka agombee ilhali wapenda majungu wanadai amewapanga wakati hakuwa na mpango wa kugombea tena nafasi hiyo.

“Mimi sikuwaza kugombea na niliwahi kukataa mara kadhaa. Nilikuwa nawaza kumpata ‘Mnyamwezi’ mwingine mwaminfu wa kumkabidhi kijiti lakini Kamati Kuu iliyokaa hivi karibuni ilinikatalia kufanya hivyo na mara kadhaa iliniomba nigombee tena,”alisema Mbowe.

Alisema hadi kufikia jana, alikuwa hajachukua fomu na kwamba alipanga siku ya leo awe safarini kuelekea nchini Uingereza.

Mbowe alijigamba kuwa kutokuwa na uelewa na weledi katika uongozi, kuliwafanya watu wengine kupotelea njiani kwa kutojua.

Alisema kuwa kuna wanaotumika na kuna walioishiwa na nguvu na hata wengine kupata fedha kuhakikisha malengo ya kuvuruga chama yanatimia lakini yeye alipambana hadi CHADEMA ikasonga mbele.

“Sikuwahi kuomba hata mara moja kugombea nafasi hii katika vipindi vyangu vitatu. Mwaka 2004, niliombwa na aliyekuwa Mwenyekiti Bob Makani, nikakataa lakini jopo la Wazee liliniomba, nikakubali.

“Mwaka 2005, pia sikuomba kugombea urais, na nafasi hiyo ilikuwa igombewe na Prof. Mwesiga Baregu ambaye mwishoni alijitoa na nikaombwa nigombee mimi,”alisema.

Kwa mujibu wa Mbowe, mwaka 2009, aliombwa tena kugombea uenyekiti na akalipiwa tena fedha za kuchukulia fomu na sasa Wazee wa Kigoma wamekuwa wa kwanza kujitokeza na kumchukulia fomu.

“Hivyo, nakubali kugombea tena kuiongoza CHADEMA kivingine, hakuna chama chochote kitakachokuwa na mtindo wa kufanya hivyo hasa katika chaguzi zake mbalimbali,”alitamba Mbowe.

Aliongeza kuwa kwa sasa atafanya kazi kubwa kivitendo zaidi na kutaka kila mwanachama kutoogopa na kutumika kwa kadri atakavyoweza ili kuhakikisha wanakijenga chama.

Mbowe alikabidhiwa fomu hiyo na Mzee Mapindo Saba kwa niaba ya wawakilishi wa Wazee wa mikoa ya Rukwa, Kigoma, Pwani, Dar es Salaam, Manyara, Iringa, Njombe, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.

Wawakilishi wanena

Akizungumza baada ya kukabidhi fomu hiyo, Mapindo Saba kwa niaba ya Wazee wa Kigoma, alismea kuwa waliamua kumchukulia fomu hiyo Mbowe, kutokana na weledi na uwezo mkubwa alionao wa kujenga chama ili kuhakikisha kinasonga mbele.

“Mbowe ni mtu mwenye mbinu safi za uchaguzi, hitajio la Watanzania, mtu mwenye kupima upepo na aliyejenga uwezo wa kuongeza idadi ya viongozi wakiwemo wabunge na madiwani.

Naye mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Kinondoni, Ester Simaya alisema Mbowe amehakikisha amekijenga chama kutoka kilivyokuwa hadi sasa kutokana na nguvu na utashi alionao katika siasa.

Mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Ilala, Peter Chacha alisema Mbowe ni hodari, mwenye upendo, mchapakazi na mwenye mshikamano, hivyo ni vyema akaungwa mkono ili kuendeleza chama hicho.

Yeye mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Temeke, alisema ilikuwa ni lazima kumchukulia fomu Mbowe kwa kuwa bado wanampenda na kwamba amefanya makubwa katika chama hicho.

Mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Pwani, Said Mazoea, alisema walinyanyasika sana kwa mkoa wao umesahauliwa na serikali na kwamba CHADEMA inaweza kuwakomboa chini ya Mbowe.

Naye mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Taifa (Bawacha), Suzan Lyimo, alisema wamemchukulia fomu Mbowe kutokana na haiba yake ya kujali wanawake hasa katika kuwapa nguvu za kugombea nafasi mbalimbali.

Alisifu mchango wake wa kuhakikisha wanapata mbunge mwanamke katika jimbo la Kawe, Halima Mdee na kwamba anaamini ataendelea kufanya hivyo kwa wanawake wengine.

Mwakilishi wa Baraza la Vijana (Bavicha), Emanuel Masonga alisema vijana wametafakari na kuona kwamba Mbowe anafaa na kwamba ndiye chaguo lao katika kusukuma gurudumu la chama.

Alisema kila binadamu ameletwa duniani kwa maana na makusudio yake lakini Mbowe ameletwa kwa ajili ya kuja kuongoza na kuwafikisha watanzania pale wanapotaka.

Naye kiongozi wa Shura ya Maimamu, Sheikh Rajabu Katimba, alisema kuwa wana imani na Mbowe kutokana na kuona juhudi zake wakati wanazunguka na UKAWA mikoani.

Alisema ni aibu nchi hii kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali lakini inashika mkia kwa umaskini wa kutupwa.

Sheikh Katimba alisema nchi hii inahitaji mageuzi na kwamba Mbowe anaweza akaifikisha pale Watanzania wanapohitaji.TANZANIA DAIMA
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: