BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSHAMBULIAJI WA CAMEROON AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA KITU KICHWANI UWANJANI KATIKA MCHEZO KATI YA JS KABYLIE NA USM ALGER NCHINI ALGERIA.


CAF yataka hatua kali kuchuliwa kwa mauaji ya mchezaji

Albert Ebosse

Mchezaji mmoja wa soka raia wa Cameroon amefariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa chake kilichorushwa kutoka kwa mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya Algeria.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 Albert Ebosse aliyekuwa akiichezea kilabu kubwa ya JS Kabylie alikuwa ameifungia timu yake bao la pekee katika mechi ambayo timu hiyo ilishindwa kwa mabao mawili kwa moja na kilabu ya USM Alger.

Kitu kilichomgonga kichwani kilirushwa baada ya mechi kukamilika,wakati ambapo wachezaji walikuwa wanarudi katika chumba cha kujianda.

Waziri wa maswala ya ndani nchini Algeria ameagiza kuanzishwa uchunguzi kuhusu mauaji hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: