JE, KUPATA HUDUMA NZURI ZA AFYA KUNAMAANISHA KWENDA KLINIKI KILA JUMA ?
MTOTO
mwenye afya analala akiwa ametulia mikononi mwa mama yake. Baba yake
amefurahi sana. Kwa kuwa tukio hilo lenye kuleta shangwe hutokia mara
nyingi sana kila mwaka, ni rahisi kuona kwamba kujifungua mtoto ni jambo
la kawaida tu. Kwa kweli, hilo ni tukio la kiasili—kwa hiyo, kwa nini
mtu awe na wasiwasi ?.
Ni kweli kwamba akina mama wengi hujifungua bila matatizo lakini haiwi
hivyo nyakati zote. Kwa sababu hiyo, wazazi wenye busara hufanya
chochote wanachoweza ili kuepuka matatizo. Kwa mfano, wao hujifunza
mambo yanayosababisha matatizo wakati wa kujifungua, wanaenda kliniki ya
akina mama waja-wazito, na wanachukua hatua rahisi za kupunguza
matatizo wakati wa kujifungua. Acheni tuchunguze baadhi ya hatua hizo
kwa undani.
Kisababishi kimoja cha matatizo kwa mama na mtoto wakati wa kujifungua
ni kukosa kujitunza vizuri mama anapokuwa mja-mzito. Dakt. Cheung
Kam-lau, ambaye ni tabibu wa watoto walio chini ya umri wa mwezi mmoja
katika Hospitali ya Prince of Wales huko Hong Kong, anasema kwamba
“kutoenda kliniki kabla ya kujifungua kunaweza kuhatarisha mimba.” Pia
anasema kwamba “wengi wa akina mama hao hutazamia kujifungua watoto
wenye afya na walionenepa, lakini mambo hayatendeki kama
walivyotarajia.”
Likizungumza kuhusu matatizo yanayoweza kuwakumba akina mama, jarida
Journal of the American Medical Women’s Association linasema kwamba
“sababu kuu zinazowafanya akina mama wengi wafe wanapojifungua” ni
kuvuja damu nyingi, mtoto kukaa vibaya tumboni, maambukizo, na kupanda
sana kwa shinikizo la damu. Hata hivyo, matibabu yanayofanya kazi
yanajulikana sana na katika visa vingi “matibabu ya kisasa . . .
hayahitaji matumizi ya vifaa tata,” linasema jarida hilo.
Pia, watoto wengi wanaweza kufaidika ikiwa matibabu yanapatikana kwa
urahisi. Jarida UN Chronicle linaripoti kwamba “asilimia 66 ya watoto
wanaokufa wanapozaliwa vingeweza kuzuiwa ikiwa akina mama na watoto hao”
wangepata matibabu “yanayojulikana sana, yanayofaa, na yasiyohitaji
vifaa tata.” Kwa kusikitisha, akina mama wengi hawajui la kufanya na
hawaendi kwenye kliniki za waja-wazito, linaripoti Shirika la Habari la
Philippines. Utunzaji Bora wa Mama Mja-Mzito na Kitoto Chake.
“Akina mama wenye afya hujifungua watoto wenye afya,” linasema jarida
UN Chronicle. Pia linasema kwamba mwanamke asipopata huduma nzuri za
afya anapokuwa mja-mzito, anapojifungua, na baada ya kujifungua, mtoto
wake pia hatapata huduma za afya.
Katika maeneo fulani, huenda ikawa vigumu kwa wanawake waja-wazito kupata huduma nzuri za afya.
Huenda
akahitaji kusafiri mbali, au asiwe na uwezo wa kugharamia huduma za
afya. Hata hivyo, ikiwezekana, mama mja-mzito anapaswa kujaribu kupata
huduma nzuri kutoka kwa mtu mwenye ujuzi wa kuwatunza akina mama
waja-wazito.
La, si lazima. Kuhusu
matatizo ya kawaida yanayowapata wanawake wakati wa uja-uzito na wakati
wa kujifungua, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) “liligundua kwamba
wanawake walioenda kliniki mara nne tu wakati wa uja-uzito” walipata
matokeo yale yale “kama wanawake walioenda kliniki mara 12 au zaidi.”
Madaktari Wanaweza Kufanya Nini ?.
Ili mama na mtoto ambaye bado hajazaliwa wawe na afya nzuri zaidi, madaktari, hasa wakunga, huchukua hatua zinazofuata:
▪ Wao huchunguza rekodi za matibabu za mama na kufanya uchunguzi ili
kuona kama kunaweza kuwa na hatari na hivyo kuzuia matatizo yanayoweza
kumpata mama au mtoto wake.
▪ Wanaweza kupima damu na mkojo ili kuchunguza mambo kama vile upungufu
wa damu, maambukizo, ikiwa damu ya mama na mtoto hazipatani, na
magonjwa. Magonjwa hayo yanaweza kutia ndani kisukari, surua ya rubella,
magonjwa ya zinaa, na ugonjwa wa figo, ambayo yanaweza kufanya
shinikizo la damu lipande.
▪ Inapofaa, madaktari wanaweza kupendekeza mgonjwa apewe chanjo dhidi
ya magonjwa kama vile homa, pepopunda, na kutopatana kwa damu ya mama na
mtoto.
▪ Pia wanaweza kupendekeza atumie vitamini mbalimbali, hasa aina fulani ya vitamini B inayoitwa folic acid.
Madaktari wanapotambua hatari zinazohusiana na mama mja-mzito na
kuchukua hatua zinazofaa, au kumsaidia mama kuchukua hatua hizo,
wanachangia afya nzuri kwa mama na mtoto wake ambaye bado hajazaliwa.
Kupunguza Hatari Wakati wa Kujifungua
“Wakati hatari zaidi kwa mama mja-mzito ni pindi anapopatwa na maumivu
ya kuzaa hadi anapojifungua,” anasema Joy Phumaphi, aliyekuwa naibu
msimamizi mkuu wa Shirika la Familia na Jamii la WHO.
Ni nini kinachoweza kufanywa ili kuzuia matatizo mabaya, kutia ndani yale yanayoweza kuhatarisha uhai, wakati huu muhimu?
Kwa kweli, hatua hizo ni rahisi, lakini zinapaswa kuchukuliwa mapema.*Hili
ni muhimu hasa kwa watu wanaokataa kutiwa damu mishipani kwa sababu
zinazotegemea Biblia au kwa wale wanaotaka kuepuka damu kwa sababu ya
hatari zake za kitiba.
Wagonjwa kama hao wanapaswa kufanya yote wanayoweza kuhakikisha kwamba
daktari au mkunga wao ana uwezo na uzoefu wa kutumia matibabu mengine
badala ya kuwatia damu mishipani. Pia, huenda ikafaa akina mama
waja-wazito wahakikishe kwamba hospitali watakamojifungua iko tayari
kushirikiana nao.
Unaweza kumwuliza daktari maswali haya mawili:
1. Utafanya nini ikiwa mama au mtoto anapoteza damu nyingi sana au ikiwa kuna matatizo mengine?
2. Utafanya mipango gani ya badala ikiwa hutakuwa karibu mama anapojifungua?
Bila shaka, mwanamke mwenye busara atamwomba daktari ahakikishe kwamba
ana kiwango cha juu zaidi cha damu kabla ya wakati wa kujifungua. Ili
kuongeza kiwango cha damu cha mgonjwa, daktari anaweza kupendekeza
atumie aina mbalimbali za vitamini B na madini ya chuma.
Pia daktari atafikiria mambo mengine mengi. Kwa mfano, mama huyu
alipokuwa akienda kliniki, je, aligundua matatizo yoyote ya afya
yanayohitaji kuzingatiwa?
Je, mwanamke huyo anahitaji kuacha kufanya kazi akiwa amesimama?
Je, anapaswa kupumzika zaidi?
Je, ni jambo la hekima kwa mwanamke huyo kuongeza au kupunguza uzito au kufanya mazoezi zaidi?
Je, anapaswa kukazia uangalifu zaidi usafi wa mwili kutia ndani usafi wa kinywa?
Uchunguzi unaonyesha kwamba mwanamke anapokuwa mja-mzito, magonjwa ya
fizi yanaweza kusababisha kifafa kinachotokana na mimba, tatizo baya
sana ambalo dalili zake zinatia ndani kupanda ghafla kwa shinikizo la
damu, maumivu makali ya kichwa, na kuvimba kwa mwili kwa sababu ya
kuongezeka kwa maji.
Kifafa kinachotokana na mimba kinaweza kumfanya mama ajifungue kabla ya
wakati unaofaa na ndicho kisababishi kikuu cha vifo vya mama na mtoto
wakati wa kujifungua, hasa katika nchi zinazoendelea.
Kwa kweli, daktari mwangalifu atakazia fikira dalili yoyote ya
maambukizo katika mwanamke mja-mzito. Na anapopata maumivu ya kuzaa
kabla ya wakati wake, atapendekeza alazwe hospitalini mara moja, jambo
linaloweza kuokoa uhai.
“Wanawake huhatarisha maisha yao ili kutokeza uhai,” anasema Dakt.
Quazi Monirul Islam, msimamizi wa Idara ya Kutunza Wanawake Waja-Wazito
ya WHO. Lakini utunzaji mzuri wakati mwanamke anapokuwa mja-mzito,
wakati wa kujifungua, na mara baada ya hapo unaweza kuzuia matatizo
mengi sana, hata kifo.
Jambo muhimu zaidi ni kudumisha afya nzuri. Kwa kweli, ikiwa unataka
kupata mtoto mwenye afya nzuri, lazima ujitahidi uwezavyo kuwa mama
mwenye afya nzuri.
Kulingana na tarakimu zilizochapishwa mnamo Oktoba 2007, mwanamke mmoja
hufa karibu kila dakika, yaani, wanawake 536,000 kwa mwaka, kwa sababu
ya matatizo yanayohusianishwa na uja-uzito.—Hazina ya Idadi ya Watu ya
Umoja wa Mataifa
“Kila mwaka watoto milioni 3.3 huzaliwa wakiwa wamekufa na zaidi ya
watoto milioni 4 wanaozaliwa hufa baada ya siku 28.”—UN Chronicle MATAYARISHO KWA AJILI YA KUJIFUNGUA.
1. Fanya utafiti mapema ili uchague hospitali, daktari au mkunga kwa hekima.
2. Mtembelee daktari au mkunga wako kwa ukawaida ili usitawishe urafiki na kuaminiana.
3. Tunza sana afya yako. Ikiwezekana, tumia vitamini zinazopendekezwa,
lakini epuka dawa zozote isipokuwa ziwe zimependekezwa na daktari.
Ni
jambo la hekima kuepuka kutumia kileo. “Ingawa watoto walio hatarini
zaidi ni wale ambao mama zao hutumia kileo kupita kiasi, bado
haijagunduliwa ikiwa kuna kiwango salama cha kileo ambacho mama
mja-mzito anaweza kutumia,” inasema Taasisi ya Marekani Inayoshughulikia
Matumizi Mabaya ya Kileo na Uraibu.
4. Ikiwa unapata maumivu ya kuzaa kabla ya wakati (kabla ya juma la
37), wasiliana na daktari wako au hospitali utakayojifungulia. Matibabu
ya haraka yanaweza kusaidia mtoto asizaliwe kabla ya wakati wake na
kuzuia matatizo mengine yanayoweza kutokea.
5. Andika uamuzi wako kuhusu matibabu ambayo ungependa. Kwa mfano,
wengi wameona inafaa kujaza mapema kadi ya mamlaka ya kudumu ya
uwakilishi (DPA). Chunguza ni mambo gani yanayokubalika kisheria katika
nchi unamoishi.
6. Baada ya kujifungua, tunza afya yako na ya mtoto wako, hasa ikiwa
mtoto alizaliwa kabla ya wakati. Mwone daktari wa mtoto mara moja
unapoona kuna tatizo.http://www.manyandahealthy.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment