BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS JAKAYA KIKWETE KUKAA SIKU SITA MKOA WA MOROGORO.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza jambo na waandishi wa habari juu ya ziara ya rais Jakaya Kikwete ya kiserikali anayotarajia kuifanya kuanzia Agosti 20 hadi 27 mwaka huu katika wilaya zote sita mkoani Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG

Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo na viongozi wenzake wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro.

Na Mtanda Blog, ,Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete anatarajia kufanya ziara ya siku sita katika mkoa wa Morogoro kuanzia agosti 20 hadi 26 katika wilaya sita zinazounda mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera alieleza kuwa Kikwete atafanya ziara ya kiserikali kuanzia agosti 20 hadi 26 mwaka huu.

Bendera alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli za maendeleo na kusalimia wananchi.

"Rais Kikwete ataanza ziara yake katika wilaya ya Ulanga kisha wilaya ya Kilombero ambapo atakagua miradi ya maendeleo."alisema Bendera.

Bendera alisema kuwa baada ya kutoka Ulanga na Kilombero agosti 23 atafanya ziara katika Manispaa ya Morogoro kisha wilaya ya Kilosa, Mvomero na kumalizia Gairo.

Mkuu huyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wote wa Morogoro kujitokeza kwa wingi ili kumlaki Rais Kikwete atakapokuwa anakagua shughuli za maendeleo na kufanya mikutano ya haradha katika wilaya hizo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: