BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS UHURU KENYATTA WA KENYA AMWAGIWA SIFA NA MAASKOFU 123 WA MAZIWA MAKUU KUWA NI MFANO WA KUIGWA NA MARAIS WENZAKE, WAACHE MANENO MATUPU NA KUTEKELEZA MAMBO KWA VITENDO.

http://sundayshomari.files.wordpress.com/2013/10/kenyas-president-uhuru-ke-010.jpg 
RAIS UHURU KENYATTA WA KENYA.
 
Baadhi ya maaskofu wa nchi za maziwa makuu wamempongeza Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa ushujaa wa kupambana na dawa za kulevya kwenye ukanda huo.


Aidha wanawataka marais wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Uganda, Burudi, Rwanda na Tanzania kuiga juhudi za Rais Kenyatta na kuachana na maneno matupu wakati raia wanaangamia na dawa hizo.



Nchi za Maziwa Makuu ni pamoja na Uganda, Burudi, Rwanda, Tanzania, Congo na Congo Brazzaville.

Katika taarifa ya maaskofu hao wanaomaliza kongamano lao jijini Arusha leo, iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, ilimpongeza Rais Kenyatta kwa kufuatia na kusimamia uteketezaji wa meli iliyokamatwa eneo la bahari ya Mombasa ikiwa imeshehena madawa ya kulevya iliyokuwa inakwenda Zanzibar.

Ilisema baadhi ya Maaskofu hao kutoka Uganda, Kenya,Congo , Tanzania na Rwanda walieelezea Tanzania kama eneo hatari na ghala la madawa ya kulevya kwenye jumuiya hiyo, wakionya kuwa iwapo meli hiyo ingelifika Zanzibar mihadarati hiyo ingelisambaa ukanda wote wa nchi hizo.

Baadhi ya maaskofu hao ni Joshua Zakaria wa Uganda, Dk Godwin Jelly kutoka Congo, Bees Runganizi wa Rwaanda, Bahati Banda kutoka Malawi, William Mwamalanga kutoka Tanzania na Boniface Mngayi wa Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo maaskofu zaidi ya 123 wanahudhuria kongamano la kutathimini mauaji ya alibino Tanzania na biashara ya dawa ya mihadarati wamelaani vikali ubutu wa serikali ya Tanzania katika kupambana na mauaji ya albino wakati wauaji wanafahamika na chanzo cha tatizo hilo kinajulikana.

Askofu Dk Jelly kutoka Congo aliomba Watanzania kumlilia Mungu kwani nchi yao si taifa la amani tena na kwamba umemebakia wimbo kwani mauaji ya albino yanayoendelea yametia doa kote duniani.

“Duniani watu wanauliza mauaji ya watu wanyonge kama albino yanafanywa na nani? Wanauliwa kila kukicha kwa nini serikali haijiuzulu kwa kushindwa kuwalinda?

Jelly: “Nawataka viongozi wa serikali ya Tanzania kuachia ngazi mara moja ili kuuonyesha ulimwengu kuwa wanachukia mauaji hayo ambayo yamewafanya watoto kuishi kwenye kambi maalumu kama watumwa ambako nako vimeripotiwa vitendo vya ubakaji, hii ni aibu kwa nchi inayo hubiri amani kila kukicha kumbe wanaua watu wasio na hatia… ni aibu kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali yake pamoja na CCM.”

Kwa upande wake Askofu Mwamalanga aliitetea serikali kuwa imejitahidi kupambana na mauaji hayo kwa kuanzisha polisi jamii iliyoleta mafanikio kwa kujenga uelewa kwa jamii wa kuachana na vitendo vya kishirikina ambavyo ndicho kiini kikubwa cha mauaji ya albino.

Askofu Mwamalanga hata hivyo ameungana na maaskofu wenzake kuhoji ubutu wa serikali wa kuwataja vigogo wa mauaji ya alibino nchini huku kesi zake zikiendeshwa kwa kusuasua jambo linaloenyesha kuwa wasimamizi wa mauaji hayo wamejificha kwenye fedha, jambo ambalo linahatarisha ustawi wa taifa. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: