BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJUMBE WA SIMU WAUA MWANAMKE MWANZA !!!! AJIMWAGIA LITA TATU ZA MAFUTA YA TAA MWILINI KISHA KUJILIPUA KWA MOTO BAADA YA KUFUMANIA UJUMBE KATIKA SIMU YA MUMEWE.

 
MKAZI wa Igombe, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, jijini hapa, Tausi Juma (22) aliyejilipua kwa lita tatu za mafuta ya taa kutokana na wivu wa kimapenzi na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, amefariki dunia.

Tausi alifariki usiku wa kuamkia jana hospitalini hapo, alipokuwa akiendelea kutibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kujiunguza na mafuta ya taa kwa asilimia 60 ya mwili wake.

Alijifanyia unyama huo Agosti 9, mwaka huu saa 2 asubuhi huko Igombe, ambapo mumuewe alimkimbiza katika Kituo cha Afya cha Karume na baadaye Sekou Toure kabla ya kumpelekea Bugando.

Akizungumza kwa njia ya simu, mume wa marehemu, Hussein Yadunia, aliliarifu gazeti hili jana kuwa mkewe amefariki dunia hospitalini hapo.

“Nimepokea taarifa sasa hivi kutoka kwa mjomba wa mke wangu kuwa mke wangu amefariki dunia, mimi nilikuwa sijaenda hospitali kama siku mbili nipo nyumbani naumwa,” alisema Yadunia.

Alisema amekuwa akisumbuliwa na kikohozi akashindwa kwenda hospitali katika siku hizo, lakini alikuwa akipokea taarifa za maendeleo ya mgonjwa kutoka kwa mjomba wa marehemu kwamba mgonjwa alikuwa akiendelea vizuri.

"Jana mjomba alikuja kuniona na aliagiza dawa ambazo zilikuwa zinatakiwa ila hatukununua wakati huo kwa sababu sikuwa na fedha na nilikuwa na mpango wa kuwachangisha Wananzego (kikundi cha kusaidiana) ili nipate fedha za kununua, lakini ndo hivyo tena amefariki," alisema Yadunia.

Mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema ni kweli mgonjwa huyo amefariki dunia kutokana na majeraha makubwa aliyokuwa nayo.

Kwa mujibu wa muuguzi huyo, Tausi alifariki usiku wa kuamkia jana lakini kabla ya kukutwa na mauti, alikuwa akiendelea na matibabu na hali yake ilikuwa ikiridhisha tofauti na alipopelekwa hospitalini hapo.

Tausi aliyekuwa amelazwa katika wodi namba tisa C hospitalini hapo, alifikia hatua ya kujimwangia mafuta ya taa lita tatu na kujilipua baada ya kukuta ujumbe wa mapenzi katika simu ya mkononi ya mumewe, tukio lililompandisha hasira na kuamua kujilipua.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: