BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIMELEA SUGU KWA DAWA YA MSETO VYAIBUKA.


MALARIA: Vimelea sugu kwa dawa ya Mseto vyaibuka

Dawa mseto ya malaria yenye dawa mbili; Artemether na Lumefantrine (ALU), kwa hapa nchini bado inaonekana kuwa na ufanisi mkubwa wa kutibu malaria.

Taarifa za hivi karibuni za kitafiti kutoka Shirika la Aya Duniani (WHO) zinasema baadhi ya nchi katika Bara la Asia zimeripoti kuwapo kwa usugu wa vimelea vya malaria dhidi ya kiambata kikuu kinachotumika katika kutengeneza dawa mseto aina zote, zikiwamo zinazotumika Tanzania. Usugu huo kwa mujibu wa ripoti ya WHO umeonekana kwa vimelea vya malaria aina ya Plasmodium falcipuram. Hiki ndicho kimelea kinachoongoza kwa kusababisha malaria duniani.

Hali hiyo inatishia uwezekano wa kuathiri matumizi ya dawa ya mseto ambayo inatumika nchini Tanzania iwapo hatua maalumu hazitachukuliwa.


Siku za hivi karibuni kumeibuka taarifa za kitafiti ambazo zilitangazwa na Shirika la Afya ya Duniani (WHO).


Jarida la afya la New England lilichapisha ripoti hiyo likieleza kuwa matokeo ya kitafiti yameonyesha kiambata cha dawa mseto kiitwacho artemisinin kimepata ukinzani toka kwa vimelea wa malaria hivyo kushindwa kuviaangamiza wakati wa kutibu malaria.


Artemesinin ndicho kiambata kikuu na mhimili mkuu wa dawa zote za mseto. Usugu dhidi ya kiambata cha dawa hii umeonekana kuenea katika maeneo ya Asia ya Kusini Mashariki.


Vimelea vya plasmodium falciparum vinavyosababisha ugonjwa wa malaria, vimeonekana kukinzana na dawa hii kutokana na mabadiliko yasiyotegemewa ya jeni katika Chembe za Urithi (DNA).


Watafiti hao waliweza kubaini mabadiliko hayo yaliovuruga mpangilio wa ndani ya DNA hivyo kukifanya kiambata cha dawa ya mseto cha Artemesinin kushindwa kufanya kazi kikamilifu.


Jeni ndio huwa na kazi ya kubeba taarifa za kiurithi ambavyo huwa kama katiba ya mwili inayotumiwa na ili kuelekeza shughuli za kufanya.


Kubadilika huku ni moja ya sababu kubwa ya kiambata cha artemisinin kuzidiwa mbinu na kushindwa kuviua vijidudu vya malaria.


Hata hivyo, kama vile haitoshi, inaelezwa kuwa jambo hili si la kushtusha kwa wanasayansi wa tiba kwa sababu mambo kama haya yanatarajiwa kutokea hasa pale dawa inapotumika kwa muda mrefu.


Miili ya vimelea hivi huweza kuizoea dawa na kujibadili na kuweza kuweka ukinzani dhidi ya dawa.


Nchi za Kusini mwa Asia ambazo ni Thailand, Cambodia, Vietinum ni moja za nchi ambazo nazo zimekuwa na ugonjwa wa malaria kama ilivyo nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.


Ingawa taarifa zaidi za tafiti huo inaonyesha kuwa katika kiwango cha dozi ya siku sita ya dawa ya artemisinin-imeonyesha kuweza kutibu katika maeneo ilipojitokeza usugu wa vijidudu hivi dhidi ya dawa hii. Ukilinganisha na dozi ya siku tatu kama ilivyo kwa kawaida.


Utafiti huu uliofanywa na jopo la wanasayansi wakimataifa ukiwahusisha wa Taasisi ya Tafiti za Magonjwa ya Mzio na Maambukizi (NIAID).


Walibainisha kuwa vimelea wa malaria aina ya Plasmodium Fulciparum walibadilika kwenye mfumo wao wa vinasaba ama DNA viitwavyo K13propeller Alelle. Mabadiliko hayo ndiyo yaliyosababisha kiambata cha dawa mseto kushindwa kufanya kazi ya kuviua.


Taarifa za utafiti huu zinaeleza kuwa bado kiambata cha Artemisinin kinaendelea kufanya vyema isipokuwa kwa wale ambao tayari wamekuwa na vimelea vilivyo na mabadiliko kwenye DNA.


Ikaonekana kwa kutoa kiwango cha dozi ya dawa kwa kurefusha kwa muda wa siku sita, imeonekana kusaidia kuathiri vimelea hao sugu.


Uangamizwaji huu wa taratibu kwa kiasi kikubwa unaambatana na hali ya vijidudu kujibadilisha katika chembe zao za urithi.


Jambo hili linadhihirisha ukweli wa tafiti hii kuwa tatizo la usugu linazidi kusambaa miongoni mwa maeneo ya Bara la Asia.


Mbali na Cambodia, ukinzani dhidi ya dawa hii umeonekana katika nchi za Thailand, Mynamar na Vietnam.


Taarifa zinaeleza kuwa ili kuweza kuzuia hali hii ni lazima pawepo na udhibiti wa tatizo hili katika maeneo haya.


Jambo lingine lililopendekezwa na wataalamu ni ile kurudia kuchunguza kwa kina miongozo ya matibabu ya malaria na pia kuendeleza tiba mpya tofauti tofauti ili kutoa wigo mpana wa matibabu.


Usugu huu wa dawa ni matokeo ya vitu mbalimbali ikiwemo matibabu yasioendana na miongozo sahihi ya kitaalamu kama ilivyokubaliwa na WHO.


Tatizo hili linaweza kuchochewa na wagonjwa kutokufuata maelekezo ya wataalamu katika utumiaji wa dawa.


Athari nyingine ni za kuwepo kwa dawa ambazo zimetengenezwa zikiwa hazina ubora unaotakiwa viwango.


Ubora wa dawa pia hutegemea kutumika katika kipindi kilichopendekezwa kitaalamu ili kuhakikisha kuwa nguvu ya sumu bado ipo kwa kiwango kinachoridhisha.


Hii siyo mara ya kwanza kwa dawa ya kutibu malaria kukumbana na ukinzani wa usugu kwa vimelea wa ugonjwa huo.


Usugu wa dawa za malaria uliwahi kutokea kwa chlorokwini, baadaye kwa dawa za fansidar na ndiyo maana miongozo ya tiba ilibadilika duniani kote.


Hata hivyo, mabadiliko ya miongozo ya kitiba hubadilika tu pale inapotokea kuwapo kwa tafiti za kutosha na kwa maeneo mengi pia baada ya WHO kupitia na kuridhia kuwa dawa inatibu kwa kiwago chini ya asilimia 60.


Usugu uliotokea katika bara la afya bado ni mapema kulichukulia ni tishio kwani hii imebainika katika eneo dogo la dunia.


Kinachohitajika ni tafiti kama hizi kufanyika katika maeneo mengi yenye ugonjwa wa malaria. Kwa nchi nyingi hususani Tanzania dawa za mseto bado zinaonekana kuwa ni zenye uwezo mkubwa wa kudhibiti malaria.


Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja anasema kuwa tayari Serikali imepata ripoti hiyo ya WHO na kuikabidhi kwa wataalamu wake ili ishughulikiwe.


“Wataalamu wetu ndio watakaoshauri nini kifanyike,” anasema Mwamaja.


Hata hivyo, anasema hadi sasa hakuna kimelea chenye usugu kwa dawa ya mseto kilichopatikana nchini.


Dawa za mseto ni nini?
Wataalamu wanapozungumzia dawa ya mseto ya kutibu malaria wanamaanisha ni muunganiko wa dawa mbili au zaidi lakini zote zikiwa zinatumia kiambata cha artemisinin.


Kwa jumla zipo aina nyingi za dawa ya mseto ambazo zote zimefuata mwongozo wa utengenezaji wa dawa mseto ulioamuliwa na WHO.


Serikali ya Tanzania iliamua iidhinishe dawa ya mseto ya coacterm ili itumike kama dawa maalumu ya kutibu malaria hapa nchini, hususan katika hospitali zake. Coartem ni muunganiko wa dawa mbili; Artemether na Lumefantrine (ALU).


Dawa hii hapa nchini ina punguzo la bei ili kuwezesha hata mwananchi wa kipato cha chini aweze kumudu kuinunua.


Mbali na dawa hiyo, zipo aina nyingine za mseto ambazo pia zimeidhinishwa na WHO ili zitumike duniani.


Miongoni mwa dawa hizo ni kama vile na Artusunate, Arinate, Artequicky, Co-Arinate, DUO-cotexin.


Kwa kawaida ALU hutumika kutibu malaria isiyo kali.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: