BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BI HARUSI ANUSURIKA KIFO HUKU MUME WAKE MTARAJIWA AKITUMBUKIA KATIKA MAJI YA MAFURIKI KISHA KUSOMBWA NA AFARIKI DUNIA.


Takriban watu 17 akiwemo bwana harusi na watoto wawili wamekufa maji baada ya boti ya uokoaji iliyokuwa imewabeba wageni kwenda kwa sherehe ya harusi kuzama katika mafuriko nchini Pakistan.

Maafisa wanasema kuwa takriban watu 22 wameokolewa huku waokoaji wakiwatafuta watu zaidi.

Msemaji wa shirika la kukabiliana na majanga amesema kuwa zaidi ya watu millioni 2 nchini humo waliathiriwa na mafuriko hayo ambayo yalisababishwa na mvua kubwa.

Maafisa wanasema kuwa takriban watu 289 wamefariki katika mafuriko hayo nchini Pakistan kufikia sasa.

Zahid Ali mwenye umri wa miaka 27,mchumba wake Mashal pamoja na wageni walikuwa katika boti hiyo iliyokuwa ikielekea katika sherehe za kundeleza harusi yao. Watu 18 waliokuwa wanakwenda kushuhudia harusi wameaga dunia

Maafisa wanasema kuwa boti hiyo iliojaa kupitia kiasi ilikuwa ikivuka mto Chenab uliofurika katikati ya mji wa Punjab eneo lililoathirika vibaya na mafuriko nchini Pakistan.

Msemaji wa huduma ya uokozi katika eneo hilo la Punjab amesema kuwa familia hiyo ilionywa kuhusu mafuriko hayo.

Bi harusi amesema kuwa alinusurika baada ya kushika mti wa stima.

Mazishi ya waathiriwa 17 yamefanyika huku waokoaji wakiendelea kuwatufuta wale waliotoweka.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: