BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JAJI ALIYEMUONDOLEA MWANARIADHA MLEMAVU KOSA LA MAUAJI KWA KUMPIGA RISASI MPENZI WAKE AKASILIKIWA NA FAMILIA YA MAREHEMU AFRIKA YA KUSINI.


Familia ya Marehemu Reeva Steenkamp.

Familia ya Reeva Steenkamp ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius imekasirishwa na uamuzi wa jaji wa kesi hiyo baada ya kumpata na hatia ya mauaji ya kutokusudia na kumuondoalea mashtaka ya mauaji.

June Steenkamp amesema kuwa mwanawe ambaye alikufa vibaya hakufanyiwa haki.

Amesema kuwa hakuamini kwamba jaji wa kesi hiyo alikubali ushahidi wa Oscar Pistorius kwamba alidhani bi Reeva Steenkamp alikuwa mtu ambaye alikuwa amevamia nyumba yao.

Hatahivyo mjombaake Pistorius alimshukuru jaji huyo kwa kumuondolea mashtaka ya mauaji mwanariadha huyo.

Oscar Pistorius ataendelea kuwa nje kwa dhamana hadi hukumu yake itakapotolewa mnamo mwezi ujao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: