BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JE WAJUA FAIDA WANAZOKOSA WANAWAKE KWA KUSHINDWA KUMNYESHA MTOTO MCHANGA KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI !!!. .


Shirika la afya duniani (WHO) linasisitiza mama kumnyonyesha mtoto kwa kipindi cha miezi sita bila kumwanzishia vyakula vingine.

WHO inaeleza kuwa baada ya miezi sita mama anaweza kumwanzisha vyakula vingine mtoto wake huku akiendelea kumnyonyesha maziwa ya mama angalau mpaka atakapofika umri wa miaka miwili au ziadi.


Pia, mtoto anyonyeshwe saa moja baada ya kuzaliwa, anyonyweshwe pale anapohitaji mara nyingi kwa kadri anavyohitaji usiku kwa mchana na mama anashuriwa kutotumia chupa kumpa maziwa mtoto.

FAIDA AZIPATAZO MAMA KWA KUMNYONYESHA MTOTO.
Maisha huwa rahisi kwa mama anaeyonyesha kwami ukilinganisha na maziwa ya fomula (yale ya kutengeneza viwandani). Maziwa ya mama hutumia nguvu kidogo kutumia au zaidi, hapo baadaye baada ya mama na mtoto kutulia na kuzoeana maziwa hutiririka kwa wingi zaidi.


Huitaji kuwa na kazi ya kusafisha chupa na chuchu yake kwa mashine maalumu za kuchemsha vyombo, ili kuua viini vya maradhi. Maziwa ya mama hayahitaji kununua, kupima wala kuchanganya, hayahitaji uamke usiku mwingi na uyapashe, maziwa ya mama hupatikana kwa haraka na kwa muda sahihi pale mtoto anapohitaji.


KUNYONYESHA KUNAOKOA FEDHA
Kwa mzazi huhitaji kununua vyombo na maziwa ya fomula, kwa mwaka inakubidi kutumia zaidi ya sh milioni 4 ili kugharamia maziwa ya fomula na vyombo, pia inaonyesha watoto wanaonyonyeshwa hawapatwi na maradhi mara kwa amra hivyo basi huokoa pesa nyingi ambazo zingetumika kwa matibabu.
KUNYONYESHA KUNAKUFANYA UJISIKIE MWENYE FURAHA
Kugusana kimwili wakati wa kunyonyesha na moto aliyezaliwa ni muhimu kwani mtoto huwa na usalama zaidi. Hupata joto sahihi na kutopata usumbufu wowote. Unapomnyonyesha panakuwa na ukaribu wa kimwili hivyo hufanya uhusiano wako na mtoto kuimarika zaidi hivyo humpa mtoto faraja na kwako pia. Pia mtoto huzoea harufu yako na kujihisi mwenye usalama. Hali hii ya mtoto hukutambua hukufanya kujihisi kupendwa na mtoto wako.
Mtindo uliobuniwa uitwao kangaroo ambapo mama humbeba mtoto kwa mfano wa mnyama kangaroo ambavyo mtoto wake, umeokoa maisha ya watoto waliozaliwa kabla ya muda na wenye uzito mdogo kwani huwapa joto, kusaidia maziwa kutiririka na pia huimarisha uhusiano wa mama na mtoto. Pia ukaribu wa kugusana kimwili husababishwa mwili kuzalisha zaidi kichocheo cha oxtoxini, kichochezi hiki kinasaidia maziwa kutiririka na kumpa utulivu kwa mama.

KUNYONYESHA KUNAKUEPUSHA NA MARADHI
Tafiti zinaonyesha kuwa kunyonyesha kunapunguza kupata magonjwa ya saratani ya matiti na vifuko vya mayai ya uzazi, kisukari cha aina ya pili na pia huondoa sonono baada ya kujifungua.
 
KUNYONYESHA NI NJIA YA MPANGO WA UZAZI
Kunyonyesha ni moja ya njia za mpango wa kiasili. Njia hii ya kunyonyesha ina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 98% katika miezi sita tangu kujifungua.

HUOKOA MUDA WAKO KAZINI
Kunyonyesha kunamwepusha mtoto na maradhi ya mara kwa mara hivyo kunaokoa muda mwingi wa kumuuguza mtoto.

FAIDA KWA JAMII
Tafiti za karibuni zinaonyesha kama 90% ya watoto wangelinyonyeshwa kwa miezi sita bila kupewa vyaakula vingine kungeweza kuzuia vifo vya watoto karibu 1000 na kuokoa vifo hivi, hivi kunajenga ustawi wa jamii na taifa la kesho.
http://www.manyandahealthy.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: