BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JENGO LA KANISA LENYE GOLOFA SITA LAMOKA NA KUUA WAUMINI 115, WENGI WAO NI RAIA WA AFRIKA YA KUSINI, NCHINI NIGERIA.

Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa watu 115 wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki baada ya kanisa kuporomoka nchini Nigeria.

Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, 16 kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.

 
Muhubiri T.B Joshua amewashangaza wengi kwa kusema aliona ndege ikizunguka jengo hilo kabla ya kuporomoka. 

Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo la 'All Nations in Lagos', ambalo linaongozwa na mhubiri T.B. Joshua.

Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.

Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe kuporomoka.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: