MWANARIADHA MLEMAVU ATIWA HATIANI NA MAHAKAMA KUU KWA KUMUA MPENZI WAKE BILA KUKUSUDIWA.
Pistorius akibubujikwa na machozi mahakamani kesi ilipokuwa inaendelea.
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp pasi na kukusudia.
Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa akatika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani.
Jaji Thokozile Masipa amesogeza muda wa mwanaridha huyo yuko huru kwa dhamana.
Pistorius atakuwa huru hadi hukumu itakapotolewa mwezi ujao, ambapo anaweza kuhukumiwa hadi miaka 15 gerezani. Oscar Pistorius ataendelea kukaa kwa mjombake alikokuwa muda wote kesi ilipokuwa ikiendelea.
Mjombake Pistorius, Arnold Pistorius amemshukuru Jaji Masipa kwa uamuzi wake wa kumuachia kwa dhamana.BBC Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp na kwamba alifanya mauaji hayo kwa kusudi.
0 comments:
Post a Comment