MWANARIADHA MLEMAVU OSCAR PISTORIUS HUENDA AKAFUNGWA MIAKA 25 JELA KWA KOSA LA KUMPIGA RISASI MPENZI WAKE AFRIKA YA KUSINI.
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amewasili mahakamamni kujua umauzi wa kesi ya mauaji ya mapenzi wake inayomkabili.
Jaji Thokosile Masipa ndiye anatayetoa uamuzi huo.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine hapo mwaka jana.
Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe Reeva baada ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.BBC
0 comments:
Post a Comment