BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS JAKAYA KIKWETE APEWA ZAWADI MAREKANI

Rais Kikwete anashanga na ukubwa wa kombe alokabidhiwa na wajumbe wa California
Rais Kikwete anashanga na ukubwa wa kombe alokabidhiwa na wajumbe wa California.

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, amesema ukuwaji wa haraka wa uchumi wa nchi za Afrika haujaweza kuwanufaisha wananchi wala wengi kwa sababu ukuwaji wa sekta ya kilimo ambayo wananchi wengi wanategemea haijakua kwa haraka.

 
Akizungumza katika jopo la wataalamu wa kimataifa lililotayarishwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani, USAID, hapa Washington siku ya Ijuma Rais Kikwete anasema, ingawa ripoti mpya ya Benki Kuu ya Dunia juu ya "Kukomesha ufukara ulokithiri na kuhamasisha ukuwaji".

Inaeleza kwamba ufukara duniani umepunguka kwa kasi mnamo miongo mitatu iliyopita, lakini anasisitiza kwamba wananchi wa Afrika hawajashuhudia mabadiliko hayo ya haraka.
http://gdb.voanews.com/B640AC40-9EF9-48B5-A1CB-782884B34887_cx12_cy6_cw86_mw1024_s_n_r1.jpgRais Kikwete awahutubia watanzania katika hafla ya "Usiku wa Jakaya", Washington DC.

Kiongozi huyo wa Tanzania, aliyewasili Marekani kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa Mataifa anasema mengi yanahitajika kufanywa ili kuweza kubadili hali hiyo kwa kuwekeza zaidi katika kilimo.


Na katika hafla nyingine iliyoandaliwa na Watanzania wanaoishi Marekani pamoja na wanachama wa chama tawala cha Tanzania cha CCM, Rais Kikwete, alieleza furaha yake kutokana na kwamba pendekezo lake la kuwataka Watanzania, hapa Marekani kuungana na kuunda vikao vya mashauriano na kusaidiana limetekelezwa kupita alivyo tarajia. 

"Usiku wa Jakaya Septemba 19 mwaka huu" ni hafla iliyoandaliwa hasa na wanachama wa CCM ili kumpongeza kiongozi wao kutokana na mafanikio aliyoyafanya mnamo miaka 10 ya utawala wake wa awamu ya nne Tanzania.
Rais wa Tanzania Kikwete akizungumza kwenye jopo juu ya kupambana na umaskini uloandaliwa na USAID
Rais wa Tanzania Kikwete akizungumza kwenye jopo juu ya kupambana na umaskini uloandaliwa na USAID

Kaika hotuba yake kwenye ukumbi wa hoteli ya JW Marriot mjini Washington, Rais Kikwete alizungumzia kwa urefu mafanikio katika miundo mbinu, kuimarishwa uchumi, elimu afya na huduma za jamii. Lakini alisisitiza kwamba lengo kuu lililobaki ni kuhakikisha maisha bora kwa wananchi wote wa Tanzania, na kupambana na ufukara.  
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: